Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido amesaini na Makandarasi Zabuni Tano za Ujenzi wa Barabara za Halmashauri, Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Wakuu wa Idara zote (CMT) jumla ya zabuni tano zilisainiwa ambazo zina thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Mia Tano Themanini na Saba. Zabuni hizo zitahusisha Matengenezo ya kawaida (Routine Maintenance ), Matengenezo ya sehemu Korofi (Spot Maintanence) na Matengenezo ya Gabion.
Katika Zabuni hizo Mkandarasi M/S Central Highway Contractors Ltd amesaini Lot 1 Zabuni ya Matengenezo ya Kawaida kwa Barabara ya Ketumbeine Junction-Gelai Lumbwa na Longido-Lesing'ita-Mairowa, matengenezo ya sehemu Korofi kwa Barabara za Lesing'ita-Mundarara na Matengezo ya Gabion kuzuia mmonyoko wa Udongo Eneo la Daraja la Mundarara.Thamani ya Mkataba ni shilingi 137,655,260/=
Pia Mkandarasi M/S Laizer Works Ltd amesaini Lot 2 Zabuni ya Ujenzi wa sehemu Korofi katika Barabara ya Mairowa-Sinonik na Matengezo ya Kalvati barabara ya Mairowa-Sininik. Thamani ya Mkataba ni shilingi 110,856,280/=
Wakati huo huo Mkandarasi M/S Milkha Singh Jawala Singh amesaini Zabuni ya Mradi wa Matengenezo ya Muda Maalum katika Barbara ya Sinya-Elerai 5km Mkataba huo una thamani ya Shilingi 87,917,080/=.Katika lot Na 4
Kwa Upande wa Mkandarasi M/S Ngulelo Supplies Service LTD amesaini Zabuni ya Mradi wa Matengenezo ya Muda Maalum katika Barbara ya Mairowa-Matale "A"- Emurtoto na ujenzi wa Kivuko (Solid Drift) barabara ya Matale"A"-Emurtoto. Mkataba huo una thamani ya Shilingi 160,927,338/= Katika Lot Na 3
Lakini pia Mkandarasi M/S Meero Contractors LTD naye ametia sahihi yake katika Zabuni ya mradi wa Ujenzi wa Mtaro wa Maji na Matengenezo sehemu Korofi barabara ya Longido Mjini. Mkataba huu una thamani ya shilinngi 90,160,083/- katika Lot namba 5
Katika tukio hilo la kipekee Mkurugenzi Mtendaji Wakili Jumaa Mhina amesisitiza kuwa ni vyema Makandarasi wakazingatia ubora na Muda wa Mikataba ili Matengenezo hayo yakamilike kwa wakati uliopangwa ili barabara hizo ziweze kutumika katika shughuli za wanachi za kuleta maendeleo katika Misimu yote ya Mwaka.
Imetolewa na Eng. H. Mshana
Imerushwa na Loth Zacharia & Joseph P Mkumbwa ICTOs
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM