Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh. Frank Mwaisumbe leo tarehe 25.03.2019 amesikiliza kero mbalimbali za wananchi katika mkutano uliofanyikaLongido mjini ,na kuudhuriwa na mamia ya wananchi waliokusanyika kumsikiliza na kutoa kero zao kwa Mkuu wao wa wilaya.Katika ziara hiyo ambayo imehudhuriwa pia na maofisa mbalimbali wa Halmsahauri ya Longido imeleta faraja kubwa kwananchi waliokuwa na hamu na shauku ya kutoa yaliyokuwa mioyoni mwao .wananchi wameeleza kero zao mbele ya Mkuu wa wilaya na wote wamepata ufafanuzi pamoja na mengine kutatuliwa hapo hapo,kero zilizotolewa na wananchi ni kama yafuatayo
1 . Madawa kukosekana kwenye vituo vya afya.Mganga mkuu wa wilaya ya longido Dr.Justice Munisi amewaasa wanachi wajiunge na mifuko ya afya ili waweze kupata huduma za madawa kwani serikali inatuma dawa kulingana na idadi ya kaya zilizo jiandikisha na mifuko hiyo ya afya ambapo amesema ni kaya 700 tu ndio zilizojiandikisha kwenye mifuko ya afya kati ya kaya 4000 za Wilaya ya Longido kwa namna hiyo ni ngumu serikali kujua mahitaji ya dawa kwa wananchi.
2 Kero ya passport za kusafiria . Wananchi wamelalamikia kuwa bei ghali inayo gharimu Tsh 30,000.katika swala hili la passport afisa uhamiaji amewaeleza wanachi kuwa hiyo sio passport bali ni hati ya dharura ambayo ni kwa muda mfupi tuu na kuwataka wanachi wanunue passport ambayo ni shilling laki moja na nusu na itadumu kwa miaka 10.Akijibu kero hii kwa wanachi mkuu wa wilaya amewaasa wananchi wanunue passport ya kusafiria inayouzwa kwa shilingi za Tanzania laki moja na nusu na itadumu kwa muda wa miaka 10 bila kusumbuliwa na mtu yeyote,” badala ya kununua passport ya shilingi elfu 30 ambayo ukisafiri mara kumi na laki 3 ni bora ununue passport ya laki na nusu ambayo utaitumia kwa miaka 10” amesema Mh Mkuu wa wilaya.
3.Kero ya Barabara za ndani ya mji .pia imetolewa ufafanuzi na ofisi wa TARURA ambapo amesema muda siyo mrefu wilaya ya longido ndani ya mji wa longido kutakua na barabara za lami katika mitaa kadhaa ambayo sawa na kilomita 5 ndani ya miaka hii miwili iliyobaki ya rais Magufuli.
4. Kero ya maji pia limezungumziwa na wananchi wamefurahi na kushukuru serikali hii tukufu ya rais MAGUFULI LA kuleta shilingi billion 15.8 kwa ajili ya maji wilayani Longido ,Mh rais wetu JOHN POMBE MAGUFULI tunakushukuru sana kwa maji na muda si mrefu Longido itakuwa kijani/ Green
5.Ardhi ,Migogoro ya ardhi wilayani lomngido imekwisha na mengine yanakaribia kumalizika kabisa ,Mheshimiwa mkuu wetu wa wilaya Frank MWAISUMBE kamwagiza afisa ardhi wilayani kuahakikisha migogoro modogo midogo ya viwanja vya wananchi vimemalizika kabisa.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM