Na Happiness Nselu.
Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya kata kutoka kata zote 20 za Wilaya ya Longido wamekula kiapo cha uadilifu leo, Agosti 4, katika ukumbi wa J.K. Nyerere, kama sehemu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.
Kiapo hicho kimetolewa mbele ya Hakimu Mkazi, Jaji Nasari, ambaye aliwataka wasimamizi hao kuzingatia viapo vyao kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki, amani na uwazi.
Akifungua rasmi mafunzo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo, Bw. Nevviling Lyimo, aliwataka wasimamizi hao kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu, kuepuka upendeleo na kusimamia kikamilifu sheria na taratibu za uchaguzi.“Uadilifu wenu ni msingi wa kuaminika kwa matokeo ya uchaguzi.
Hivyo ni wajibu wenu kuhakikisha mchakato mzima unafanyika kwa uwazi na kwa maslahi ya taifa,” alisema Bw. Lyimo.Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwajengea uwezo wa kiutendaji wasimamizi hao kuelekea siku ya kupiga kura.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.