Waziri wa Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh Seleman Jaffo leo tarehe 25-05-2019 ametembelea hospitali ya wilaya inayojengwa katika wilaya ya Longido kwa fedha zilizotolewa na Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli, hivi karibuni Mh Rais alitoa shillingi billion 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ili kuondoa adha ya wananchi wa Longido kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya upasuaji hasa kwa akina mama wajawazito. Katika ziara hiyo Mh waziri Jafo amefurahishwa na ujenzi wa hospitali ya wilaya iliyoanza tuu hivi karibuni mwezi wa tatu na jumla ya majengo saba tayari majengo mengi yashakuwa sehemu ya lenta tayari kwa upauaji.
Katika ziara hiyo Mh amewapongeza na kuwasifia viongozi wa wilaya pamoja uongozi wa halmashauri kwa kazi nzuri na umoja walionao katika kuhakikisha shughuli ya hospitali inaendelea kwa kasi kubwa .
“Mimi naomba niwapongeze dc na timu yako yote naomba niwapongeze,na miradi yote Longido huwa sipati shida mmejitahidi sana kuanzia mwezi wa tatu tuu mmefikia hatua hii. Mimi naomba niwapongeze hii ndio team work inayotakiwa nawapongeza sana na nina furaha sana endeleeni kufanya kazi matumaini yangu mpaka tarehe 30 mwezi wa sita iwetayari ili mwanzoni mwa mwezi wa saba Mh Rais aje kufungua kwa pamoja .” alisema Mh Jaffo.
Hata hivyo Mh Jaffo amewaahidi fedha zingine takribani million mia tano(500 million) kwa ajili ya ujenzi majengo mengine ya hospitali ya wilaya
Pia Mh Jaffo ameagiza kituo cha afya cha Eworendeke kifunguliwe kwa ajili ya kutatua matatizo ya afya kwa wilaya ya Longido,kituo cha afya cha eworendeke kimejengwa na serikali na tayari kimekamilika kwa kutoa huduma za afya wa wakazi wa kimokowa na vijiji vyake ikiwemo eworendeke na vijiji vya jirani.
Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya ya longido Mh Frank James Mwaisumbe, amepokea pongezi hizo kwa furaha na kumsifia Mh waziri Jafo kwa kazi nzuri anayofanya, Pia ameshukuru sana serikali ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuwakumbuka wakazi wa Longido kwa kuwajengea Hospitali ya wilaya itakayotatua matatizo mengi ya wilaya ikiwa ni pamoja umbali mrefu wa kufuata huduma za afya kama upasuaji hasa kwa akina mama wajawazito.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM