Na Johnson Ismail
Approved By Joseph Peter Mkumbwa. ICTO
Serikali imedhamiria kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama Wilayani Longido kwa kuanzisha Mradi mkubwa wa maji kutoka katika chanzo cha Mlima Kilimanjaro hadi kufika katika makazi ya wananchi.
Waziri Kasim Majaliwa Kasim Ameweka jiwe La msingi leo kwaniaba ya Dr.John Pombe Magufuli kwenye Mradi Mkubwa wa Maji wilayani Longido.
Hatahivyo Mh.Kasim Majaliwa ameipongeza serikali ya awamu ya Tano kwa utekelezaji wa mradi huu kwani utawanufaisha wakazi wa longido kwa kiasi kikubwa, pia alimtaka Mhandisi Ramadhani Msiba kuongelea miradi ya Maji inayo endelea wilayani na kumambia hata Mhamisha hadi miradi yote itakapo kamilika kwani ni Mchapakazi vizuri.
Aidha Mhandisi ramadhan msiba ameelezea utekelezaji wa Mradi huu mkubwa kua umegawanyika katika miradi midogo midogo minne ,ambayo ni kutoka chanzo kikuu hadi Longido mjini,kinachogharimu jumla ya shilingi billioni10,890,000,000,Utekelezaji wa pili wa ni ukarabati wa matanki mawili makubwa yaliyopo Longido mjini na kupeleka maji katika kijiji cha Engikareti kitakachogharimu jumla ya shilingi bilioni 2,539,752,938.Utekelezaji wa tatu ni Ujenzi wa Tanki kubwa Longido mjini lenye ujazo wa lita laki 450 utakaogharimu kiasi cha shilingi 276,355,771.20 na mradi wa mwisho ni kusambaza mabomba kilomita 44.9 Longido mjini utakaogharimu shilingi bilioni 2,087,830,435.00.
Vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni pamoja na Engikareti,Oltepes,Orbomba,Longido na Ranchi vyenye jumla ya idadi ya Wakazi elfu 29.
Pia Mhandisi Msiba alitaja jumla kuu ya fedha zinazo gharim mradi huu hadi kukamilika kwamba ni15,766,897,539660. Mradi unatarajia kukamilika mwakani 2018 na ametaja miradi mingine inayo endelea vijijini ikiwa ni jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa maji Wilayami longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM