Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb), ameongoza uzinduzi rasmi wa chanjo ya mifugo katika Wilaya ya Longido, mkoani Arusha, hafla ambayo imehudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenani Kihongosi, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi, na jamii.Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa J.K. Nyerere, wilayani Longido,
Waziri Kijaji aliwahimiza wafugaji kubadili mtazamo wa ufugaji wa kizamani na kuanza kufuga kwa njia za kisasa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mifugo inapatiwa chanjo kwa wakati na inatambuliwa rasmi kupitia mifumo ya utambuzi wa kitaalamu.“Ni lazima tuwekeze katika afya ya mifugo yetu kwa kuwapatia chanjo na kuzitambua. Hii itawawezesha wafugaji wetu kushiriki kwenye masoko ya kimataifa na kuongeza kipato,” alisema Dkt. Kijaji.
Baada ya mkutano, Waziri Kijaji alitembelea eneo la Engikareti, lililoandaliwa kwa ajili ya zoezi la uchomaji chanjo, ambapo mifugo ilichanjwa kupitia njia maalum ya cattle crush (eneo la kupitishia mifugo kwa ajili ya matibabu na chanjo). Eneo hilo pia ni sehemu ya kunywesha maji mifugo na si josho kama ilivyozoeleka.
Waziri alitumia fursa hiyo kusisitiza matumizi ya miundombinu bora kama cattle crush kwa ajili ya huduma endelevu za afya ya mifugo, akisema kuwa hilo ni mojawapo ya hatua muhimu katika kuimarisha mifumo ya ufugaji wa kisasa.Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh.Kenani Kihongosi, aliwahimiza wafugaji wa Longido kujitokeza kwa wingi katika kampeni za chanjo, akibainisha kuwa serikali ipo bega kwa bega na wafugaji kuhakikisha wanapata huduma bora.“Longido ina mifugo mingi lakini tunahitaji mifugo bora na yenye afya ili iweze kutumika katika uchumi wa kisasa. Serikali itahakikisha mazingira yanakuwa rafiki kwa wafugaji,” alisema Kihongosi.Chanjo hiyo ni sehemu ya mikakati ya serikali ya kukabiliana na magonjwa sugu ya mifugo, kuongeza uzalishaji.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM