NA ABRAHAM NTAMBARA
Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) limetoa mafunzo kwa Viongozi wa Dini, Vijiji na viongozi wa Kimila kuhusu Sera mbalimbali za utunzaji wa mazingira wilayani Longido.
Akizungumza katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza leo Oktoba 15, 2025 wilayani Longido chini ya Mradi wa Faith4Restoration, Kiongozi wa Mradi huo kutoka WWF Prof. Noah Sitati alisema ni kwa mara ya kwanza wanatumia viongozi wa dini katika kuelemisha utunzaji wa mazingira.
Profesa Noah amesema Kwamba wameamua kuwatumia viongozi hao, kwasababu wamekuwa wakaeneza injili, hivyo anaamini itakuwa ni rahisi kupenyeza elimu ya utunzaji wa mazingira kwa waumini wao.
Alisema elimu hiyo wameanza kuitoa katika Vijiji vitatu ambavyo ni Orbomba, Kimokouwa na Eworendeke, hata hivyo alibainisha kuwa baadaye wataipeleka katika vijiji vingine.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi Faith4Restoration kutoka WWF Ofisi ya Arusha Jane Shuma alisema wanawapa mafunzo hayo kwasababu wao ndio watakaoshiriki katika utekelezaji wa mradi.
"Lengo la kuwashirikisha Viongozi wa Dini, Vijiji na Kimila ni kuhakikisha wanatoa mchango katika suala la utunzaji wa mazingira," alisema Shuma.
katika mafunzo hayo watawapitisha kwenye maeneo matatu ambayo ni kuhusu uondoshaji wa mimea vamizi, utunzaji wa vyanzo vya maji na mmomonyoko wa udongo uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Naye Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Bi. Sofia Gashomba, alisema Longido kwa sehemu kubwa imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame, hivyo mafunzo hayo yatasaidia katika utunzaji wa mazingira.
Kwamba viongozi hao watasaidia kutoa elimu kwa wananchi ili kuendelea kutunza mazingira kwa kuacha kukata miti na uchomaji mkaa hali ambayo itasaidia kurejesha uoto wa asili.
Aidha Sheikh wa Wilaya ya Longido Ramadhani Mpangala aliishukuru WWF kwa kuwashirikisha katika mafunzo hayo ya utunzaji wa mazingira.
Sheikh Mpangala alisema hata Dini inasema kuwa mazingira ni uhai, hivyo elimu wanayoipata kwenye Semina hiyo, wataipeleka kwa waumini wao.
Kadhalika Kiongozi wa Kimila na Mwenyekiti wa Nyanda za malisho Kijiji cha Eorendeke Lucus Sambeke alisema mafunzo ambayo wamekuwa wakipatiwa yamekuwa na faida kubwa kwani yameshaanza kuleta matokea kwa kuanza kurejesha uoto wa asili.
Alisema kuwa kama vingozi wamekuwa wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi ya utunzaji wa mazingira kwa kuwataka kuacha kukata mita na kuwahimiza kupanda miti.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.