Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya wizara ya mifugo ,kilimo na maji leo tarehe 20/03/2019 wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maji na mifugo katika halmashauri ya Wilaya ya Longido.Ziara hii iliyoongozwa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge katika wizara ya mifugo,kilimo na maji Mheshimiwa Mohamood Mgimwa ilitembelea miradi mitatu ambayo ni
1: Mradi mkubwa wa maji wa mto simba uliogharimu shilingi za kitanzania billion 15 wenye uzo wa kuhudumia wakazi laki moja na nusu.Kisima cha maji kina uwezo wa kubebe lita laki nne na nusu ambazo zitaondoa kabisa adha ya maji kwa wakazi wote wa wilaya ya longido ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kwa sababu ya maji kwa ajili ya mifugo yao pamoja na matumizi yao binafsi.akizungumza katika ziara hiyo mwenyekiti wa kamati ya maji ambaye ni Mbunge wa Mufindi kaskazini Mh Mohamood Mgimwa amewaasa wananchi wa wilaya ya Longido kutunza miundo mbinu ya maji ili iweze kuwasaidia katika kukabiliana na ukosefu wa maji ,aidha amewaagiza wakandarasi wanao sambaza maji katika vijiji vyote wahakikishe wanawaondolea wananchi shida ya maji katika kila kijiji ambacho bomba la maji limepita ili wananchi wawe watunzaji wa miundo mbinu hiyo ya maji kwani itakuwa rahisi kwao kutunza.
2: Mnada wa kimkakati wa Mifugo wa Eworendeke wenye viwango vya kimataifa uliogharimu takribani million 700.
Kamati imeweza kutembelea mradi wa mnada wa Eworendeke uliojengwa na MIVAF ,Halmashauri ya longido pamoja na serikali kuu mradi huu ulianza mwaka 2016 ukiwa chini ya Halmashauri lakini mwaka jana 2018 serikali kuu kupitia wizara ya mifugo ilikuja kwenye mnada huu na kuanza kukusanya mapato pamoja na Halmashauri Katika mnada huu kamati ilishauri wizara ya Mifugo kupitia kwa Naibu waziri Abdalah Ulega kuhakikisha inapunguza kodi ambayo kwa sasa ni shilling elfu 35 ambayo imekuwa kikwazo kikubwa sana kwa wafanya biashara wa ng’ombe wanaopeleka mifugo nchi jirani ya Kenya ili kuweza kurejesha wafanya biashara ambao wamekuwa wakitorosha mifugo yao kupeleka Kenya badala yake warudi kwenye mnada wa ndani waendelee kufanya biashara ili kuinua uchumi wa ndani .Aidha kwa upande mwingine kamati imeshauri Wizara ya Mifugo na serikali kuu kuangalia tena mgawanyo wa mapato ambao Wizara imekua ikichuwa fedha zote za makusanyo na kuacha Halmashauri na kiasi kidogo ambapo kwa ngombe mmoja Wizara wanachukua shilling elfu 34000 na kuacha Halmashauri na shilingi elfu moja tuu.kamati imeshauri Wizara ikubali kugawana aslimia 50 kwa 50 na Halmashauri hii ambayo tegemeo lake kubwa ni mifugo ili iweze kupata mapato kwa ajili ya kuendesha ya Halmshauri, kamati ya bunge imeamua kulichukua swala hili ambalo ni kanuni ya wizara ya mifugo kama marekebisho yaweze kufanyika kwani ni wanancjhi ndio wanao umia ambao ndio lengo kuu la serikali kuwahudumia wao na sio kuwaumiza.
3: Kiwanda cha nyama wilaya ya longido yenye uwezo wa kuchinja ngombe 200-500 kwa siku pamoja na mbuzi 2000 kwa siku.katika ziara hii kamati ya bunge ilipokea taaarifa ya kiwanda kipya kabisa cha nyama hapa wilayani longido ambacho kinategemewa kuanza kazi rasmi mwezi october mwaka 2019 na kuajiri wanachi karibu mia nane na kupunguza kabisa tatizo la ajira kwa wakazi wa Longido na watanzania kwa ujumla.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM