Waheshimiwa Madiwani na baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido wamefanya Ziara ya mafunzo tarehe 15/9/2022 katika Halmashauri ya TUNDUMA na ziara hiyo ilihusu namna bora na yenye tija ya ukusanyaji mapato katika vyanzo mbali mbali vya halmashauri.
Waheshimiwa madiwani na Wataalamu kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri ya Tunduma wametembelea miradi mbali mbali ikiwepo maegesho ya magari,ushuru wa mpakani, mashine ya kufyatulia tofali pamoja na shule ya msingi yenye mchepuo wa kingereza inayomilikiwa na Halmashauri.
Mh.Mwenyeki wa Halmashauri ya Longido Mh. Saimon Oltesoi amewashukuru sana watumishi na madiwani wa Tunduma kwa namna walivyotoa mafunzo hayo kwa weredi na ustadi mkubwa ambako ameahidi kufanyia kazi yale yote yalioelekezwa kwa lengo la kuongeza mapato katika halmashauri ya wilaya ya Longido
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido ndg.Stephen Ulaya amewaomba watumishi pamoja na madiwani kusimamia na kutumia njia nzuri ya makusanyo ya mapato pamoja na kubuni vyanzo bora na vyenye tija katika kupandisha ama kuongeza mapato katika halmashauri"sasa ni wajibu na ni jukumu letu sisi kama halmashauri kuona haja ya kuongeza usimimizi wa mapato ndani ya halmashauri yetu ili kuisadia serikali kupata fedha zitakazo Saidia kuleta maendeleo kama shule hospital barabara maji,umeme hivyo basi niwaombe ndugu zangu tushirikiane kwenye kutekeleza jambo hili kwa maslah mapana ya nchi yetu"Alisema ndugu Stephen Ulaya
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM