Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Mh.Daktari Charles Msonde amefanya ziara yake Wilayani Longido Tarehe 14/05/2024 akitokea nchini Kenya alipohudhulia Mashindano ya riadha ya watoto wenye Umri wa Miaka 12 hadi 15 ambapo watoto walioshiriki Mashindano hayo kutoka Tanzania wameibuka kidedea kwa kushika nafasi ya Tatu kati ya nchi ishirini na moja zilizoshiriki Mashindano hayo huko Nairobi Nchini Kenya.
Mheshimiwa Dkt Msonde alipata wasaa mzuri wa kuzungumza na Watumishi wa Kada ya Elimu Msingi na Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.
Dkt Msonde amewataka wasonge mbele na kufanya Kazi kwa bidii huku Serikali ikiendelea kutatua kero na changamoto zao zinazofifisha utendaji kazi wao.
Changamoto hizo Dkt Cherles Msonde amezigawa katika sehemu sita zikiwemo Kucheleweshwa kwa upandaji wa madaraja,Ucheleweshwaji wa kubadilishiwa Muundo, Malimbikizo ya Mshahara, Kutopatiwa kwa wakati fedha za nauli na fedha za uhamisho (posho ya kujikimu), sambamba na majibu yasiyoridhisha kwa baadhi ya viongozi wanapotaka kupatiwa huduma au kuomba kupatiwa ufumbuzi wa kero zinazowakibili.
Mbali na uwepo wa Changamoto hizo Dkt Msonde amewaambia walimu kuwa; tayari Serikali kwa kushirikiana na Wizara husika wameshazibainisha kero hizo na Kero nyingi kwa kiasi kikubwa zimeshatatuliwa na zilizo salia zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi. Na amewaahidi walimu waliofika kwenye kikao /Mkutano huo kuwa ni Lengo na Mkakati wa Serikali mara tu ifikapo Tarehe 01/07/2024 kero zote za watumishi hao zitakuwa zimetatuliwa na madeni yao yote yatakuwa yameisha.
Aidha Dkt.Msonde amewaagiza Maafisa Elimu Msingi na Sekondari kuwa karibu na walimu ili waweze kubaini kwa haraka changamoto na kero zinazowakabili kwa lile linaweza kutatulika wajitahidi wanashughulikia kwa haraka sana ili walimu hao waweze kufanya kazi kwa weredi na utulivu.
"Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan anawapenda sana walimu na anajitahidi sana kutatua kero zinazowakabili walimu na anataka tuchape kazi bila kudharauliana na kama tu mashahidi wengi wetu hapa madaraja yamepanda, miundo imebadilika na Madeni ya walimu walio wengi yamelipwa na kwa wachache ambao bado tumeagiza Maafisa utumishi waliopo kwenye Halmashauri zenu na waliopo Ofisi kuu yaani Tamisemi kuchambua upya madai ya mwalimu mmoja mmoja ili waweze kupata stahiki zao". Alisema Dkt. Msonde.
Nae mwalimu Pantaleo Paleso amemshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Tamisemi anaeshughulikia maswala ya Elimu kwa kupata wasaha mzuri wa kuzungumza na walimu pamoja na kuwatia moyo. Sisi kama walimu tunaahidi Serikali yetu kwamba tunakubali kufanya mabadiliko katika Elimu yetu ya Tanzania na tunahakika matokeo yetu ya mitihani yetu yote kuanzia darasa la Nne mpaka ya kidato cha sita yatakuwa na ufaulu wa juu, ili kuweza kupata Taifa Imara na la wasomi.
Akizungumza kwa Niaba ya watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw. Nassoro Shemzigwa amemuahidi Naibu katibu mkuu kuwa watashirikiana bega kwa bega na watumishi sambamba na kujitahidi kutatua changamoto zao makazini.
LONGIDO TUNATEKELEZA KWA VITENDO#
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM