Mheshimiwa dkt Festo John Dugange Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Leo tarehe 6/03/2023 amefanya ziara katika miradi mbali mbali ikiwemo shule ya Sekondari Mundarara, kituo cha Afya cha Ketumbeine, Oworendeke, na kuhitimisha kwenye hospital ya Wilaya ya Longido ambako bado ujenzi wake unaendelea kwa baadhi ya majengo machache ili kukamilisha ujenzi huo.
Mheshimiwa Naibu waziri ameiagiza kamati ya wilaya pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama wahakikishe wanakamalisha miradi yote kwa haraka ili iweze kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.
Mheshimiwa naibu waziri pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa wilaya pia amesisitiza matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na Serikali hususani pesa za miradi zinatumika kwenye miradi iliyokusudiwa na serikali na si vinginevyo na kukamilika kwa muda uliopangwa.
Naye mkuu wa wilaya ya Longido ndugu Marko Henry Ng'umbi kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Longido ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wake Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuona ipo haja ya kutoa fedha nyingi kwenye miradi ya Afya pamoja na shule ili iweze kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Longido ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata changamoto za huduma hizo muhimu.
"Kwa kipindi kirefu wananchi wa wilaya ya Longido imewalazimu kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo muhimu. Uwepo wa hospital hizi zitawasaidia sana wananchi wote wa Wilaya yangu hasa kina mama ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu mahala pazuri na salama pakujifungulia sasa serikali imewesogezea huduma ya mama na mtoto kwa karibu hivyo nadhahiri kuwa kina mama wote watapata huduma bora za kujifungua bila tatizo lolote kwa usawa na usalama zaidi"Alisema mkuu wa wilaya.
Sambamba na hilo mheshimiwa mkuu wa wilaya ameahidi kutekeleza na kufuatilia kwa karibu ukamilishwaji wa baadhi ya miradi yote yenye changamoto na kuahidi kukamilisha kwa wakati na muda uliowekwa, pia amemshukuru Naibu waziri Dkt Festo John Dugange . Kwa kuridhia kutembelea miradi iliyopo Wilayani humo kwani itasaidia na kuongeza chachu na hali ya ukamilishwaji wa miradi kama ilivyo pangwa.
kwa ziara hii Mheshimiwa naibu waziri wananchi wa wilaya ya Longido na vitongoji vyake inatambua kuwa serikali ipo karibu na wananchi wake hususani wa jamii hii ya wafugaji.
Tunaomba utufikishie salamu zetu za dhati kabisa kwa Rais wetu Mama yetu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza na kuipa kipaumbele wilaya yetu, zaidi sana tunakuomba Mheshimiwa Naibu Waziri usichoke kuja kututembelea mara tu upatapo nafasi"Alihitimisha kwa kusema hayo ndugu Simon Oltosoi Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Longido.
*Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee*
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM