• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Mifugo na Uvuvi



Mkuu wa idara ya Mifugo na Uvuvi. Ndg.Nestrory Dagharo  

Namba ya simu  0782749201



Kiasi cha asilimia 95 ya eneo la Wilaya ya Longido linatumika kwa ufugaji na wanyamapori. Kati ya hekta 778,200 za Wilaya eneo la malisho ni hekta 639235 (tazama jedwali 1). Wilaya ina Ng’ombe 216,575  wa 

nyama na ng’ombe wa maziwa 273, Mbuzi wa nyama 399,754, kondoo 301,211, Kuku 15,666, Punda 15,339, Nguruwe 153 na  Mbwa 15,012 na Ngamia 180.

  • Jedwali 1: Mgawanyo wa Ardhi

Matumizi 

Eneo (KM za Mraba)

Hekta

%

Eneo linalotumika kwa Kilimo

292.23

29223

3.76

Eneo la Malisho

6392.35

639235

82.14

Eneo linalofaa kwa Kilimo

731.75

73175

9.4

Misitu

365.75

36575

4.7

Jumla Eneo la Wilaya

7,782

778,200

100

  •  
  •  
  •  
  •  

MIUNDOMBINU YA MIFUGO

Wilaya ina miundombinu mbali mbali kwa matumizi ya mifugo ikiwa ni pamoja na majosho, mabwawa, malambo, vibanio, mabirika, minada na machinjio. Hali ya miundombinu ya mifugo ni kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini;

Jedwali 2: HALI HALISI  YA MIUNDO MBINU YA MIFUGO

AINA
MAHITAJI
IDADI ILIYOPO
MAZIMA/IMARA
 
MABOVU
UPUNGUFU
Majosho
64
24
11
12
41
Mabwawa
72
9
8
-
63
Malambo
120
25
25
-
95
Vibanio
96
45
45
-
51
Mabirika
96
48
48
-
48
Machinjio
2
2
2
-
-
Minada
11
11
2
9
9

 

1.2 HALI HALISI YA WATUMISHI WA UGANI MIFUGO

Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jumla ya watumishi 21 kati ya 64 wanaohitajika, upungufu 43 wanaohitajika kulingana na huduma zinazohitajika katika kata 18 na vijiji 49 vya Wilaya. Aidha jumla ya Maafisa Ugani wa Mifugo 14 wapo ngazi ya Kata, kati yao 11 wana usafiri wa pikipiki.

Katika kuboresha/kuimarisha upatikanaji wa huduma za ugani Wilaya imewapatia Maafisa Ugani 12 pikipiki na magari 2 yapo Makao Makuu ili kuimarisha utendaji kazi katika maeneo yao. Pikipiki hizo zinasaidia Maafisa Ugani kuwafikia wafugaji na kuwafundisha mbinu za ufugaji bora.  Hii imesaidia kuboresha Mifugo na kuongeza uzalishaji.

1.3 HALI YA HEWA

Wilaya ya longido ni moja ya Wilaya iliyopo kwenye nyanda kame hapa nchini. Wilaya inapata wastani wa mvua kiasi cha 500mm maeneo ya ukanda wa chini na 900mm maeneo ya ukanda wa juu kwa mwaka, kama kuna mtawanyiko mzuri wa mvua. Wakati mwingine hupata wastani wa 500mm kwa mwaka wenye uhaba wa mvua.

1.4 FURSA ZILIZOPO

Wilaya ina fursa ya kuwekeza kwenye sekta ya Mifugo hasa biashara ya mifugo na mazao yake. Mifugo wa Longido hasa ng’ombe, mbuzi na kondoo wameboreshwa kwa asilimia 65 hivyo kuna fursa kwenye uwekezaji kwenye mifugo na mazao yake.

Wilaya ina eneo kubwa la nyanda za malisho linaloweza kuendelezwa lenye ukubwa wa kilometa za mraba 6392.35 eneo ambalo likipata fedha za kuwekeza katika kukarabati/kuboresha nyanda za malisho itasaidia mifugo kupata malisho ya kutosha kwa mwaka mzima.

  • MAENDELEO YALIYOFANYIKA KATIKA SEKTA YA MIFUGO
  • VYAMA VYA USHIRIKA WA WAFUGAJI
  • Wilaya kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya Kiserikali ya TRIAS na ‘African Wildlife Foundation’ imeanzisha na kuwajengea uwezo wanachama wa vyama 8 vya Ushirika wa Wafugaji katika kata 8 za Ketumbeine, Elang’atadapash, Gelai Lumbwa, Meirugoi, Ilorienito, Kamwanga, Olmolog na Tingatinga zilizopo katika tarafa za Enduimet na Ketumbeine. Vyama hivyo vinaendelea na shughuli za kunenepesha ng’ombe na biashara.
  • Kuanzishwa kwa Ushirika wa Wafugaji kutasidia kupata nguvu ya soko la mifugo na pia kuhamasisha jamii ili kuondokana na mila ya kutouza mifugo wakati wakiwa na hali nzuri. 
  • 2.2 CHANJO YA MIFUGO 

Wilaya ikishirikiana na wadau mbali mbali imekuwa na harakati endelevu za kupambana na magonjwa mbali mbali ya mifugo ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

  • Jedwali 3: CHANJO NA TIBA YA MIFUGO
HUDUMA 
UGONJWA
AINA YA MIFUGO ILIYOCHANJWA
IDADI YA MIFUGO ILIYOCHANJWA
Chanjo
Upele wa Ngozi kwa ng’ombe
Ng’ombe
129,967
Chanjo
Ndigana Kali
Ng’ombe
88,423
Chanjo
Homa ya Mapafu kwa ng’ombe
Ng’ombe
123,987
Chanjo
Kichaa cha mbwa
Mbwa
4,178
Chanjo
Kideri
 Kuku
8,098
  •  
  •  
  • UNENEPESHAJI NA VIKUNDI VYA KIUCHUMI
  • Katika kuongeza thamani ya mifugo na mazao yake juhudi za kuboresha mifugo ya asili na kunenepesha inaendelea kufanyika kupitia Vikundi 13 vya unenepeshaji katika Kata za Engarenaibor, Mundarara, Engikaret, Tingatinga na Olmolog. Jumla ya ng’ombe 360 tayari wamenenepeshwa na kuuzwa. Kazi ya ununuzi, uuzaji na uzalishaji ni endelevu kwa vikundi. Uwezeshwaji wa vikundi hivi umefanywa na Halmashauri pamoja na taasisi za Utafiti na Mafunzo hasa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na shirika la ‘African Wildlife Foundation’. Aidha jumla ya shilingi 172,674,000/= kupitia Mipango ya Maendeleo  ziliwezesha vikundi hivyo kuendelea na shughuli za unenepeshaji.

Elimu ya ufugaji bora unaozingatia utaalamu imetolewa kwa vikundi 50 vya wafugaji ambavyo 15 ni vya unenepeshaji wa ng’ombe katika Kata 8 na jumla ya madume 360 yalinenepeshwa na kuuzwa, vikundi 64 ni vya Wanawake kwa ajili ya ufugaji wa bora wa kuku chini ya mradi wa maisha bora ili kuwawezesha kuinua pato lao kutokana na mifugo. Aidha kupitia mradi wa Maisha Bora unaofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji vijiji 8 vyenye jumla ya vitongoji 35 vimenufaika na kila kikundi kitapata madume bora kwa vikundi vya wanaume na wanawake watapata mbuzi na kuku.

  •  
  • PROGRAMU YA MIVARF
  • Wilaya kupitia Programu ya ‘MIVARF’ itajenga mnada wa mpakani na miundombinu ya machinjio katika kijiji cha Eworendeke. Mradi upo katika hatua za mwazo za utekelezaji. Bajeti iliyotengwa kwa mradi ni Tsh.1,000,000,000/=. Ujenzi huo utakapokamilika mwishoni mwaka 2016 utasaidia upatikanaji wa soko la mifugo.
  • MIFUGO YA KIFUTA MACHOZI

Wananchi wa Longido bado wanaendelea kuishukuru Serikali kwa kupata mradi wa Mifugo ya Kifuta Machozi ili kukabiliana na janga la ukame lililotokea mwaka 2008/2009. Katika mpango wa kutoa Mifugo ya Kifuta Machozi, Wilaya iliidhinishiwa jumla ya Tshs. 5,704,000,000/= kwa ajili ya ununuzi wa Ng’ombe 11,408 na Mbuzi 14,260 kwa ajili ya kaya 2,852 zilizopoteza mifugo yao yote.  Hadi 2016, jumla Tshs. 2,989,000,000 zilikwishatolewa na kutumika katika ununuzi wa Ng’ombe na mbuzi ambapo ng’ombe 6,805 na mbuzi 3,340 tayari waligawiwa kwa kaya 1,701.  Mradi huu umesaidia sana familia zilizopoteza mifugo yote na kuweza kurudi tena kwenye shughuli zao za kiuchumi za ufugaji. 

UBORESHAJI WA MIFUGO

 Katika jitihada za kuboresha mifugo wa asili Wilaya kwa kushirikiana na wadau hasa mashirika yasiyo ya Kiserikali CORDS, PWC imewanunulia Wafugaji madume bora ya ng’ombe 65, mbuzi na kondoo 50. Aidha Wafugaji wenye uwezo wanaendelea kujinunulia wenyewe madume bora.

  • Kiujumla uboreshaji wa mifugo kwa kutumia madume bora umefikia asilimia 60 kwa mbuzi na kondoo na asilimia 40 kwa ng’ombe.  Jamii imehamasika na inaunga mkono kwa kupewa ushauri wa kitaalum kupitia Watumishi wa Ugani wa Mifugo walioko kwenye kata.
  •  
  •  
  •  
    • Dume Bora la Mbegu
     
    •  
     
    • Mbuzi walioboreshwa (Aina ya Isiolo) wakiwa Malisho

       

      •  
      • Kondoo Walioboreshwa  kwa Madume Bora aina ya Black Head Persian

         

        • MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI
      • Vijijji vyote 49 vya Wilaya vina mpango wa matumizi bora ya ardhi na maeneo ya malisho yameainishwa kwa kila kijiji. Maeneo ya hifadhi ya malisho kiasili yameainishwa na kutunzwa kulingana na taratibu za kimila.

         

                    3.0 CHANGAMOTO

        • Wilaya ya Longido inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na:-
        • Uhaba mkubwa wa upatikanaji wa maji kwa mifugo hasa kipindi cha kiangazi.
        • Ukomo wa bajeti: Fedha kidogo zinazotolewa kwa ajili ya idara ya mifugo kutotosheleza mahitaji halisi ya ujenzi wa miundombinu ya maji hasa mabwawa.
        • Upungufu wa Maafisa ugani wa Mifugo katika ngazi ya Kata na Vijiji.
      • 4.0 MIKAKATI /UTATUZI WA CHANGAMOTO

        Wilaya ina mikakati/mipango mbali mbali kuendeleza sekta ya mifugo kama ifuatavyo:-

        Kuomba kwenye bajeti ya kila mwaka kuajiriwa Maafisa Ugani Mifugo.

        Kuhamasisha wenye mifugo wengi kuwa na malambo kwenye maeneo yao.

        • Kuboresha mifugo na mazao yake kupitia mipango mbalimbali ya maendeleo kila mwaka.
        • Kuchanja na kutibu mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali.
        • Kushirikiana na wadau kuboresha nyanda za malisho na miundombinu ya mifugo.
        • Kuelimisha wafugaji juu ya matumizi endelevu ya nyanda za malisho na miundo mbinu ya mifugo kama vile vibanio, majosho na mabwawa.
        • Kuendelea kutoa mafunzo/huduma za ushauri kwa Wafugaji kupitia Maafisa Ugani.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM