• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Maendeleo ya jamii


UTANGULIZI:

Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa divisheni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido, na ni kiungo muhimu kati ya Halmshauri na Jamii kwa kuratibu na kusimamia shughuli za kimaendeleo. Divisheni ya maendeleo ya jamii ina Jumla ya watumishi 15 ambapo wanaume 10 na wanawake 5 wanaotoa huduma kwa ngazi ya Wilaya na kata. Ambapo makao makuu ya willaya kuna watumishi 7 (me 3 ke 4) ngazi ya kata watumishi 8 (me 7 ke 1).

MALENGO LA DIVESHENI YA MAENDELEO YA JAMII

Kujenga uwezo wa jamii endelevu, kwa kuwezesha jamii katika kubaini mahitaji yao, kubuni, kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya kujiletea maendeleo kwa kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo kwa kujipatia na kujiongezea kipato kwa kuimarisha hali ya maisha ya jamii.

MUUNDO WA DIVISHENI

Divisheni ya maendeleo ya jamii inaongozwa na mkuu wa divisheni chini ya wasaidizi wawili ambao ni Mkuu wa sehemu ya masuala ya mtambuka na Mkuu wa sehemu ya mashirika yasiyo ya kiserikali. Chini ya sehemu mbili za Divisheni kuna Madawati tano ambayo ni:-  Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi na kupunguza umaskini,Dawati la uratibu wa kupambana na maambukizi ya ukimwi, Dawati la maendeleo ya jinsia na mtoto,  dawati la ushirikishwaji wa jamii na dawati la uratibu, ufuatiliaji na usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGOS. Majukumu ya jumla ya Divisheni na madawati husika yameainishwa kama ifuatavyo:

MAJUKUMU YA JUMLA YA DIVISHENI YA MAENDELEO YA JAMII.

  • Kushirikisha Jamii katika kuainisha fursa na changamoto zinazoikabili ili kulijiletea Maendeleo.
  • Kuelimisha Jamii kuondokana na Fikra, Imani, Mila, Desturi na Tamaduni Zinazokinzana na Maendeleo.
  • Kushirikisha Jamii katika Kuwaunganisha na Kuwawezesha makundi Maalum katika fursa na Mchakato wa Maendeleo ili kuinua ustawi wao.
  • Kuratibu Utekelezaji na Uzingatiaji wa Masuala ya Jinsia Katika Programu na Mipango ya Maendeleo Katika Sekta Mbalimbali.
  • Kuwezesha Jamii Kutumia Fursa ya Sera za Kisekta na Mikakati yake katika Kujiletea Maendeleo.
  • Kuwezesha Wananchi Kunufaika na Fursa za Kiuchumi.
  • Kuwezesha Jamii Kutekeleza Haki na Malezi ya Mtoto.
  • Kuwezesha Usajili, Kuratibu na Ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
  • uwezesha Jamii Kutambua, Kuanisha na Kuzuia Migogoro inayoathiri Maendeleo katika Jamii
  • Kuratibu na Kuhamasisha Ushiriki wa Jamii katika Masuala Mtambuka.
  • Kutoa Elimu ya Haki na Wajibu wa Jamii na Kuwezesha Uratibu na Usajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria Katika Ngazi  Wilaya
  • Kuelimisha Jamii Faida za miradi mikubwa ya kitaifa Kwa maendeleo ya Taifa na fursa Kwa jamii

   MAJUKUMU YA MADAWATI

  • DAWATI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NA KUPUNGUZA UMASKINI
  • Kushirikiana na Kamati ya Uwezeshaji ya Hamashauri kutekeleza Mkakati wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi;
  •  Kuhamasisha wananchi kujiunga na SACCOS na VICOBA kwa lengo la kujiwekea akiba na kupata mitaji;
  •  Kuchambua fursa zilizoko katika Miradi mikubwa ya uwekezaji na miradi ya Kitaifa na kuelimisha wazawa ili waweze kushiriki/kuajiriwa;
  • Kuratibu utoaji wa mikopo inayotokana na asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kuwezesha wanawake, vijana na watu wenye ulemavu;
  • Kuhakikisha Halmashauri inatenga maeneo maalum ya uwekezaji kiuchumi kama vile kilimo, viwanda na biashara ndogondogo na za kati; na
  •  Kufuatilia utekelezaji wa shughuli za uwekezaji kiuchumi katika Halmashauri na kuandaa taarifa ya utekelezaji.
  • DAWATI LA URATIBU WA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI,
  • Mafunzo ya VICOBA kwa watu wanaoishi na virus vya UKIMWI(WAVIU)
  • Kuhakikisha tathmini ya hali halisi ya VVU na UKIMWI katika Halmashauri inafanyika na kuweka mikakati ya Kila mwaka.
  • Kuhamasisha kuunda
  • Kutoa taarifa za shughuli za VVU na UKIMWI kwenye kikao cha kamati ya UKIMWI
  • Kupitiaa taarifa za uratibu zinazofanywa na Kata na Mitaa ili kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha na kuongeza ufanisi.
  • Kuratibu, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli za VVU na UKIMWI zilizopangwa.
  • Kutambua na kutathmini shughuli za wadau mbalimbali wanaotekeleza afua za VVU, na UKIMWI katika Halmashauri. Vikundi vya WAVIUna wajane.
  • Kuhakikisha mipango yote ya UKIMWI na wadau wanaotekeleza katika Halmashauri inaingizwa kwenye Mpango Mkakati wa UKIMWI wa Halmashauri na Mkoa ili kuondoa urudufu wa juhudi na rasilimali.
  • Kuhakikisha sera, Mkakati wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, sheria, Miongozo na matokeo ya tafiti mbalimbali ya masuala ya UKIMWI yanawafikia wadau na wananchi kwa ujumla.
  • Kutoa ushauri kwa ngazi inayohusika kuhusu Sera au sheria ndogo juu ya udhibiti wa VVU na UKIMWI.
  • Kuhakikisha uwepo wa orodha ya wadau hai wa Masuala ya UKIMWI.
  • DAWATI LA MAENDELEO YA JINSIA NA MTOTO
  • Kuratibu program za haki na Maendeleo ya Mtoto zinazotekelezwa na wadau ili kuhakikisha zinafuata Sera, Sheria za Serikali na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa iliyolenga Haki za Mtoto.
  •  Kuhamasisha na Kuelimisha familia, jamii na wadau katika kuwekeza kwenye malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ili kuwa na jamii bora iliyojengwa kwa misingi ya umoja na mshikamano wa kitaifa.
  • Kuunganisha nguvu za wadau mbali mbali wanaofanya kazi za watoto ili kuepusha migongano na matumizi mabaya ya rasilimali fedha na watu.
  • Kuhakikisha ukatili dhidi ya watoto unatokomezwa kupitia mipango na program za kitaifa ambazo zimeandaliwa kwa kushirikiana na wadau.
  •  Kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala ya haki, ulinzi na ustawi wa mtoto kupitia uelimishaji umma kwa kutumia vipindi vya redio za jamii, runinga, maadhimisho, mikutano na midahalo.
  •  Kuratibu ukusanyaji, uhuishwaji, uchambuzi na usambazaji wa takwimu zinazohusu watoto.
  • Kuratibu uanzishwaji na uendeshaji wa mabaraza ya watoto katika ngazi ya kijiji, Kata, na Wilaya.
  • Kuratibu uanzishwaji na uendeshwaji wa vikundi vya malezi kwa familia katika ngazi ya jamii.
  •  Kuanzisha na kufuatilia matumizi ya rejista ya matukio ya uvunjifu wa haki za watoto na namna yalivyoshughulikiwa katika ngazi ya kijiji, Kata na Halmashauri.
  • Kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia katika Halmashauri yanatambuliwa kwa kufanya uchambuzi wa jinsia (gender analysis).
  •  Kuhakikisha masuala ya jinsia yanaingizwa katika mipango ya vijiji, Mitaa na Halmashauri.
  • Kuwezesha mafunzo mbali mbali ya jinsia kwa kadri ya mahitaji.
  • Kutoa rufaa kwa wahanga wa ukatili wa jinsia (Ustawi wa Jamii, Polisi, Wanasheria na Hospitali).
  • DAWATI LA USHIRIKISHWAJI WA JAMII
  • Ushirikishaji jamii kutambua fursa na vikwazo kwa maendeleo ili kupendekeza njia sahihi ya kutatua kwa kufanya utafiti wa kawaida na utafiti shirikishi.
  •  Ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu za uchumi na kijamii na za mchanganuo wa jinsia zitakazotumika wakati wa kutoa maamuzi na upangaji mipango na bajeti, ufuatiliaji na tathmini;
  •  Uhamasishaji wa jamii katika kuandaa au kuhuisha mipango shirikishi na bajeti ya mwaka kwa kuzingatia vipaumbele.
  • Ushiriki wa jamii katika kuanzisha, kutekeleza na kusimamia miradi ya jamiii na shughuli za kujitegemea kwa kutumia rasimali zilizopo kwenye jamii na kutoka nje.
  •  Uandaaji na usambazaji wa jumbe rahisi zinazoelimisha jamii kuhusu Mikataba ya Kimataifa, Sera na dhana mbalimbali za maendeleo na maelekezo ya Serikali Mfano Tanzania ya viwanda, Ugatuaji Madaraka, Elimu Bure, Mabadiliko ya Tabia Nchi n.k
  • Kuandaa ujumbe rahisi wa kuelimisha jamii kuwa na mtizamo chanya kwenye miradi mikubwa ya Kitaifa ya Gesi, Umeme, Maji,
  •  Kuratibu shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
  • MAJUKUMU YA DAWATI LA URATIBU, UFUATILIAJI NA USAJILI WA NGO’s
  •  Kuwezesha Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyopo katika Halmashauri.
  •  Kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyopo katika Halmashauri.
  • Kufuatilia shughuli, miradi na program zinazotekelezwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kubaini kama zinawafikia na kuwanufaisha walengwa.
  •  Kuandaa taarifa kuhusu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Yaliyopo Katika halmashauri na kuiwasilisha kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
  • Kuratibu Uwasilishwaji wa mpango kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuingiza/kuhuisha katika mipango na bajeti za Wilaya.
  •  Kutatua changamoto mbali mbali ikiwemo migogoro inayokabili Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyo ndani ya halmashauri
  • Kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2001, Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24/2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 na Kanuni mbali mbali za usajili na uratibu wa Mashirika haya nchini.
  •  Kutoa ushauri wa wadau kuhusu usajili, ufuatiliaji na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa Mashirika na wadau mbali mbali kwenye halmashauri.
  •  Kuwezesha na kukuza ushirikiano kati ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini, Serikali na wadau mbali mbali wa maendeleo.
  •  Kusimamia chaguzi za viongozi wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi husika.
  •  Kuhamasisha uanzishaji wa mitandao ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi ya eneo husika kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano miongono mwa mashirika haya.
  •  Uratibu wa Vikundi vya maendeleo vya Kijamii (CBOs).
  • Kuratibu Watoa huduma za Msaada wa Kisheria katika Jamii.

      HUDUMA ZITOLEWAZO NA DIVISHENI YA MAENDELEO YA JAMII.

  • Cheti za Utambuzi wa Vikundi.
  • Taratibu za usajili wa NGO’S na utambulisho wa NGO’S.
  • Vipengele Muhimu katika uandaaji wa Katiba
  • Kupokea wanafunzi wa Field (Mafunzo kwa vitendo)
  • Fomu mbalimbali anazopewa Mwananchi kujaza anapotaka huduma.
  • Utoaji wa Mikopo

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.