• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Maliasili na uhifadhi wa mazingira

1. UTANGULIZI

Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido ni miongoni mwa vitengo muhimu vinavyosimamia na kuratibu shughuli zote zinazohusiana na utunzaji wa rasilimali za asili, mazingira na maendeleo ya utalii. Kitengo hiki kina jukumu la kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali hizi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kitengo hiki kinaongozwa na Afisa Maliasili na kinahusisha seksheni nne (4) ambazo ni:

  1. Seksheni ya Uhifadhi wa Wanyamapori
  2. Seksheni ya Misitu
  3. Seksheni ya Mazingira
  4. Seksheni ya Ufugaji wa Nyuki

2. VIVUTIO VYA UTALII WILAYANI LONGIDO

2.1 Uwepo wa Spishi mbalimbali za Wanyamapori

Wilaya ya Longido imezungukwa na hifadhi mbalimbali kama:

  • Pori la Akiba la Pololeti
  • Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA)
  • Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA)
  • Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya
  • Hifadhi za jamii upande wa Kenya katika maeneo ya mpaka wa kimataifa

Sehemu kubwa ya Wilaya ni mapito ya wanyamapori kutoka mashariki kwenda magharibi na kinyume chake, hali inayochochea utalii wa picha na uwindaji wa kitalii. Wanyamapori hupatikana hata karibu na makazi ya watu, hali inayorahisisha upatikanaji wa vivutio kwa gharama nafuu.

Kwa sasa, Wilaya ina jumla ya vitalu 7 vya uwindaji vinavyomilikiwa na wawekezaji waliopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

2.2 Mbuga ya Engasurai – Enduimet WMA

Eneo hili linalojulikana kama "Serengeti Ndogo" linapatikana ndani ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Enduimet. Watalii wanaweza kuona:

  • Twiga, pundamilia, nyumbu, swala wa aina mbalimbali, digidigi, tembo
  • Ndege wakubwa kama mbuni, tandawala na ndege secretary
    Ni eneo bora kwa utalii wa picha, utalii wa ndege, na tafiti za kisayansi.

2.3 Spishi za Ndege

Longido imebarikiwa kuwa na aina nyingi za ndege wa kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi. Hili ni eneo linalofaa kwa bird watching na tafiti za kitaaluma.

2.4 Ziwa Natron

Ziwa hili ni kivutio maarufu duniani kutokana na sifa za kipekee:

  • Mazalia ya Flamingo: Ni makazi muhimu ya ndege heroe wadogo (lesser flamingo) kutokana na mazingira ya chumvi na alkalini.
  • Mandhari ya kipekee: Maji hubadilika rangi kuwa nyekundu au waridi kutokana na kemikali na viumbe wa majini.
  • Utalii wa Ikolojia: Watalii huweza kutembelea nyayo za binadamu wa kale, kufanya matembezi ya asili, na kutembelea misitu ya Ketumbeine na Gelai.

2.5 Mlima wa Volkano wa Oldoinyo Lengai

Ni mlima pekee wenye volkano hai inayopoa na kutoa maajabu ya kijiolojia. Huvutia watalii wa kupanda mlima na wanasayansi.

2.6 Utalii wa Kitamaduni

Jamii ya Kimasai imehifadhi utamaduni wake kwa miaka mingi. Watalii hupata fursa ya:

  • Kutembelea maboma
  • Kushiriki shughuli za kijadi
  • Kujifunza maisha ya kila siku ya jamii ya Kimasai

3. SEKSHENI ZA KITENGO NA MAJUKUMU YAKE

3.1 Seksheni ya Uhifadhi wa Wanyamapori

Majukumu:

  1. Kusimamia uhifadhi wa wanyamapori ndani na nje ya hifadhi.
  2. Kufanya doria za mara kwa mara na kushtukiza kudhibiti ujangili.
  3. Kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi na ufugaji wa wanyamapori.
  4. Kushughulikia changamoto za wanyama waharibifu na hatari.
  5. Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha katika vitalu.
  6. Kufuatilia vifo vya wanyamapori na kuchukua hatua stahiki.

3.2 Seksheni ya Misitu

Majukumu:

  1. Kusimamia na kulinda misitu ya asili na iliyopandwa.
  2. Kuratibu upandaji miti na kampeni za utunzaji wa mazingira.
  3. Kutoa elimu kuhusu umuhimu wa misitu kwa jamii.
  4. Kusimamia matumizi endelevu ya misitu kwa kutoa vibali.
  5. Kufanya doria dhidi ya uvunaji haramu wa mazao ya misitu.
  6. Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu mashamba ya miti.

3.3 Seksheni ya Mazingira

Majukumu:

  1. Kufanya tathmini ya athari za kimazingira kwa miradi yote (EIA).
  2. Kutoa elimu kwa jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira.
  3. Kuratibu matukio ya mazingira (Siku ya Mazingira Duniani, Tuzo ya Raisi n.k).
  4. Kutoa elimu ya udhibiti wa magugu vamizi kama Parthenium, Ipomea, Prosopis.
  5. Kuratibu upandaji wa miti na uhifadhi wa vyanzo vya maji.
  6. Kufanya ukaguzi wa mazingira katika viwanda na migodi.
  7. Kuhamasisha matumizi ya nishati safi.
  8. Kufanya tafiti za mazingira kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali.
  9. Kushirikiana na mashirika ya ndani na nje katika utekelezaji wa miradi ya mazingira.

3.4 Seksheni ya Ufugaji wa Nyuki

Majukumu:

  1. Kutoa elimu juu ya ufugaji bora wa nyuki na uchakataji wa mazao.
  2. Kuratibu uanzishaji wa vikundi vya wafugaji wa nyuki.
  3. Kusimamia miradi ya ufugaji wa nyuki kwa vikundi na mtu mmoja mmoja.
  4. Kutoa mafunzo ya kuongeza ubora wa mazao ya nyuki kwa ushindani wa soko.
  5. Kuelimisha jamii juu ya nafasi ya nyuki katika uhifadhi wa mazingira.
  6. Kusaidia vikundi vya nyuki kupata vyeti, mafunzo na masoko.

5. MIKAKATI YA KITENGO KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

Kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira katika mwaka wa fedha 2025/2026, kitengo kimejiwekea mikakati ifuatayo:

  1. Kuimarisha doria za uhifadhi katika maeneo ya wanyamapori, misitu na mazingira ili kudhibiti ujangili na uharibifu wa maliasili.
  2. Kuhamasisha na kuongeza ushiriki wa jamii katika shughuli za uhifadhi kupitia uanzishaji wa vikundi vya mazingira, nyuki, na ufuatiliaji wa wanyamapori.
  3. Kupanua maeneo ya upandaji miti kwa kushirikiana na shule, taasisi na jamii ili kuchangia kampeni ya Taifa ya kupanda miti.
  4. Kutekeleza kikamilifu tathmini ya athari za mazingira (EIA) kwa miradi mipya ya maendeleo inayopangwa kutekelezwa ndani ya Wilaya.
  5. Kuwezesha vikundi vya vijana na wanawake kushiriki katika miradi ya ufugaji wa nyuki na utunzaji wa mazingira kupitia mafunzo na mikopo midogo.
  6. Kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala (safi) kama majiko banifu, gesi, na umeme wa jua ili kupunguza ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa.
  7. Kufuatilia kwa karibu magonjwa, vifo na uhamaji wa wanyamapori na kuandaa taarifa za mara kwa mara kwa wadau husika.
  8. Kuimarisha ushirikiano na mashirika ya ndani na nje ya nchi katika kutekeleza miradi ya uhifadhi wa mazingira, ikolojia na utalii wa jamii.
  9. Kuratibu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa kushirikisha shule, taasisi na wananchi kwa ujumla.
  10. Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria ndogo za mazingira katika vijiji na kutoa ushauri kwa ajili ya maboresho ya sheria hizo.
  11. Kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya utalii wa picha na utalii wa kitamaduni, kwa kushirikiana na sekta binafsi, kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri.
  12. Kuweka mfumo wa kielektroniki wa taarifa za mazingira na rasilimali za asili kwa urahisi wa ufuatiliaji na upangaji wa mipango.
  13. Kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradi ya mazingira iliyotekelezwa katika mwaka uliopita na kuandaa ripoti ya mapendekezo kwa ajili ya kuboresha mipango ijayo.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.