Wilaya ya Longido ni miongoni mwa wilaya sita (06) za Mkoa wa Arusha, kaskazini mwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jina “Longido” limetokana na Mlima Longido, ambao kwa lugha ya Kimasai huitwa Loongiito, likimaanisha “mlima wenye mawe ya kunolea visu.” Wilaya hii ina eneo la kilomita za mraba 8,180.
Kijiografia, Wilaya ya Longido imezungukwa na mifumo mikubwa ya ikolojia inayochangia umuhimu wake kama mazalia, malisho na mapito ya spishi mbalimbali za wanyamapori. Upande wa mashariki inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) iliyounganishwa na Ushoroba wa Kimataifa wa Kitenden (Kitenden Wildlife Corridor). Kusini inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA), magharibi na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) pamoja na Pori la Akiba la Pololeti, huku kaskazini ikipakana na Hifadhi ya Taifa ya Amboseli nchini Kenya.
Mbali na mandhari yake ya kipekee, Wilaya ya Longido imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, vikiwemo spishi zaidi ya 40 za wanyamapori, aina mbalimbali za ndege wakiwemo Heroe wadogo (Lesser Flamingo) wenye mazalia Ziwa Natron, Mbuni (Ostrich), Tandawala (Kori Bustard) na Ndege Sekretari (Secretary Bird) pamoja na urahisi wa kufikika maeneo mengi ya vivutio. Mchanganyiko huu wa rasilimali na fursa unaiweka Longido katika nafasi ya kipekee kama kitovu cha shughuli za utalii kaskazini mwa Tanzania.
Jedwali Na.1. Baadhi ya wanyamapori wanaopatikana Wilayani Longido.
| Jina la kawaida
|
Spishi
|
| Tembo
|
Loxodonta Africana
|
| Nyati
|
Syncerus caffer
|
| Twiga
|
Giraffa Camelopardalis
|
| Simba
|
Panthera leo
|
| Duma
|
Acinonyx jubatus
|
| Chui
|
Panthera pardus
|
| Mbwa Mwitu
|
Lycaon pictus
|
| Digidigi
|
Madoqua kirkii
|
| Pofu
|
Tragelaphus oryx
|
| Mbuzi mawe
|
Oreotragus oreotragus
|
| Swala pala
|
Aepyceros melampus
|
| Swala Granti
|
Grant gazelle
|
| Tandala kubwa
|
Tragelaphus strepsiceros
|
| Tandala mdogo
|
Tragelaphus imberbis
|
| Choroa
|
Fringed Eared Oryx
|
| Mbuni
|
Struthio camelus
|
| Fisi madoa
|
Crocuta crocuta
|
| Fisi Mraba
|
Hyaena hyaena
|
| Swala thomi
|
Eudorcas thomsonii
|
| Ngiri
|
Phacochoerus africanus
|
| Nyumbu
|
Connochaetes taurinus
|
| Pundamilia
|
Equus quagga
|
| Swala Twiga
|
Litocranius walleri
|
| Kori Bustard
|
Ardeotis kori
|
| Heroe wadogo (Lesser Flamingo)
|
Phoeniconaias minor
|
Uwindaji wa Kitalii (Tourist Hunting):
Hii ni aina ya uvunaji wa wanyamapori madume yaliyozeeka unaofanywa na Wawindaji Wageni chini ya usimamizi wa Serikali kwa lengo la Utalii (Consumptive Wildlife Utilization). Mgeni anapaswa kulipia ada ya vibali na wanyama kupitia Kampuni inayomiliki Kitalu husika cha Uwindaji kabla ya kusafiri kutoka nchi yake kuja nchini Tanzania kwa Shughuli za Uwindaji. Aina hii ya Uwindaji, inafanyika katika maeneo maalum yaliyotengwa na Serikali kama vitalu vya Uwindaji kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii. Aidha, mwishoni mwa mwaka 2022, Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia mnada wa Kielectroni (Electronic Auctions), iligawa Vitalu saba (07) vya Uwindaji Wilayani Longido kwa Kampuni sita (06) za Uwindaji kama inavyosomeka kwenye Jedwali Na.2. hapo chini.
Jedwali Na.2. Orodha ya Vitalu vya Uwindaji Wilayani Longido na Kampuni zinazomiliki.
| S/N
|
JINA LA KITALU
|
KAMPUNI INAYOMILIKA
|
MUDA WA UMILIKI
|
|
|
Pori Tengefu Ziwa Natron Kaskazini.
|
Adam Clements Safaris Ltd.
|
2023 - 2032
|
|
|
Pori Tengefu Ziwa Natron Kusini.
|
Robin Hurt Safaris Ltd.
|
2023 - 2032
|
|
|
Pori Tengefu Ziwa Natron Magharibi.
|
Kilombero North Safaris Ltd.
|
2023 - 2032
|
|
|
Pori Tengefu Ziwa Natron Mashariki.
|
Green Mile Safaris Co. Ltd
|
2023 - 2042
|
|
|
Pori Tengefu Longido Kaskazini.
|
Michel Mantheakis Safaris Ltd
|
2023 - 2032
|
|
|
Monduli Juu Open Area.
|
Tanzania Big Game Safaris Ltd.
|
2023 - 2032
|
|
|
Eneo la Uwindaji la Engasurai-EWMA
|
Kilombero North Safaris Ltd.
|
2023 - 2032
|
Utalii wa Picha (Photographic Tourism):
Hii ni aina ya utalii usio wa uvunaji (Non-Consumptive Wildlife Utilization) unaofanywa na wageni kwa kutembelea vivutio vya Utalii ndani ya Wilaya yetu kwa lengo la kupiga picha na kutazama wanyamapori katika mazingira yao. Wageni wengi hufika Longido kutazama Wanyamapori mbalimbali na ndege pamoja na kupanda mlima Longido wenye urefu wa mita 2,637 kujionea mandhari tambarare za mbuga zinazozunguka Mlima Kilimanjaro na Meru.
Utalii wa Kitamaduni (Cultural Tourism):
Longido ni kitovu cha Utalii wa Kitamaduni ambapo wageni wanaweza kutembelea maboma ya Wamasai kwa Lengo la kujifunza kuhusu mila, tamaduni na maisha ya kila siku ya Jamii ya Wamasai. Wageni wataweza kupata fursa ya kupiga picha ya matukio halisi ya jamii hiyo kama wanawake wakiokota kuni, watoto wakichunga mifugo, na usanifu wa kipekee wa boma za Wamasai (nyumba za makazi).
Kwa maelezo na msaada zaidi fika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Longido, au
piga simu namba :
0784889889 Afisa Wanyamapori Wilaya,
0787115234 Afisa Utalii Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.