Kwa kutambua umuhimu na thamanj ya Ardhi Halmashauri ya wilaya ya Longido mkoani Arusha imeanzisha mpango shirikishi wa urasimishaji na kampuni ya iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya makazi ya Geoid Geomatics Consultants Enterprises.
Idara ya Ardhi imepanga kufanya zoezi hilo la urasimishaji wa makazi holela kwa maeneo ya Namanga na Longido ikishirikiana na Kampuni hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti hususani mapato ya ndani.
Afisa Ardhi Bi.Letara ameeleza kuwa pamoja na kwamba mkataba huo wa Halmashauri na kampuni husika haujasainiwa lakini idara yao imejitahidi kufanya uhamasishwaji wa wananchi wa eneo la Namanga kwa kuwa sisitiza kuwa Ardhi iliyo pimwa ni mali hai na ardhi ambayo haijapimwa nia mali mfu kwa maana ya kuwa haitambuliki na serikali pindi utakapohitaji msaada kama vile mkopo.
Vilevile Bi.Letara amesema wananchi kwa upande wao wameonesha moyo na mwitiko mkubwa katika zoezi hilo la upimaji ardhi kwani wameelimishwa kuhusiana na umuhimu wa upimaji ardhi ikiwa ni kuweza kupata mkopo benki,kuepuka msongamano wa makazi katika eneo moja ,kurahisisha zoezi la usafirshaji kutokana na uwepo wa barabara.
Pia amesema kuna mwongozo chini ya sheria na mamlaka ya ardhi unaoeleza kuwa kila mwananchi anatakiwa kutenga sehemu ya eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa barabara na kuwajibika kumchangia mtu ambaye atakuwepo katika eneo stahiki kwa ajili ya barabara kwa kumfidia gharama zake za ujenzi na eneo atakalo jengea makazi yake upya.
Aidha kamati hiyo imetoa mapendekezo ya gharama za urasimishaji ikiwa ni kupanga,kupima ,kuchonga barabara na mgawanyo wa mapato kulingana na ukubwa wa kiwanja kama ifuatavyo ukubwa wa kiwanja 1.<150 mita sguare ,ni sh.276000, 2.(151___300) meter sguare ni sh.310000, 3.(301___800)meter sguare ni sh.380000, 4.(1501___1500)meter sguare ni sh.495000 na 5.(1501___2500 ni
Sh.625000.
Pia wamependekeza kuwa kampuni itafanya kazi zote za kupanga,kupima,kuainisha ,kuchonga barabara na kuwajibikaji kulipa fidia zote zitakapo hitajika kwa zoezi la utekelezaji kusimamiwa na halmashauri na mgawanyo wa mapato ni 10% kwa halmashauri kuratibu na kusimamia mradi, 10% kwenye kata na 80% inayobakia kwenye kampuni ikiwa ni gharama za urasimishaji na fidia itakapohitajika .
Hivyo basi ili kazi ianze rasmi Halmashauri itaandaa mkataba wa kisheria wa makubaliano hayo utakao sainiwa na pande zote husika na kazi hiyo
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM