Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ni Kamati inayoshughulika na masuala ya uzalishaji mali ikiwemo Kilimo, Mifugo, Viwanda, Madini, Biashara pamoja na Miundombinu na suala zima la Maendeleo ya Ardhi na hifadhi ya Mazingira.
kupendekeza kwa Halmashauri mipango ya kupanua biashara na jinsi ya kukusanya mapato yatokanayo na upanuzi huo
kupendekeza mipango ya matumizi ya Ardhi katika Halmashauri
kusimamia matumizi ya Sheria ya Nguvu kazi
kuandaa mipango madhubuti ya upanuzi wa Maendeleo ya Kilimo
kusimamia na kuhakiki miradi ya Ujenzi wa masoko, minada, majosho na vituo vya Mifugo
kushughulikia uanzishaji na uendelezaji wa Vyama vya Ushirika
kupendekeza mipango ya Ujenzi au upanuzi wa Vituo, viwanja, majengo na Mazingira ya burudani, starehe, mapumziko na michezo
kuamua juu ya mambo yanayohusu uhifadhi wa mambo ya kale na mandhari mbalimbali zenye sura nzuri
kuandaa na kuratibu njia bora juu ya uhifadhi wa Nyaraka muhimu kwa ajili ya Kumbukumbu kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 287
kupendekeza namna bora ya malezi ya Vijana ili waweze kuwa wazalishaji katika Taifa
kusimamia uanzishaji wa uendelezaji wa Vikundi vya Jamii na vya hiari vya wananchi katika Halmashauri kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Jamii
kusimamia na kuhakiki maeneo ya Misitu, Mapori na Mbuga zilizotengwa kama Hifadhi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa
kupendekeza na kufanya tathmini ya uendelezaji wa mabonde, mito na mabwawa
kubuni na kupendekeza namna ya kudhibiti Moto
kubuni na kupendekeza mikakati ya utumiaji wa Nishati mbadala, kuzuia ukataji wa Miti ovyo na kuhimiza upandaji miti kwa wingi
kuhakikisha kwamba Ukaguzi wa Majengo unafanyika mara kwa mara
kupendekeza Sheria Ndogo zinazohusu Kamati hii
WAJUMBE WA KAMATI YA UCHUMI, UJENZI NA MAZINGIRA KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018
NA
|
JINA |
KATA |
CHAMA |
1
|
MHE. PETER LEKANETI
|
TINGATINGA - MWENYEKITI
|
CCM
|
2
|
MHE. SABORE K. MOLLOIMET
|
MWENYEKITI WA HALMASHAURI
|
CCM
|
3
|
MHE. DR STEPHEN KIRUSWA
|
MBUNGE
|
CCM
|
4
|
MHE. WITNESS ISACK
|
VITI MAALUM – TINGATINGA
|
CCM
|
5
|
MHE. HASSAN NGOMA
|
NAMANGA
|
CUF
|
6
|
MHE. JAMES K. KUKAN
|
MATALE
|
CCM
|
7
|
MHE. NAOMI E. MOLLEL
|
VITI MAALUM – LONGIDO
|
CHADEMA
|
8
|
MHE. SANO OLTUS
|
ILORIENITO
|
CCM
|
9
|
MHE. LODUPA S. LAITAYOK
|
KIMOKOUWA
|
CHADEMA
|
10
|
MHE. MOTIKA KASOSI
|
ORBOMBA
|
CCM
|
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM