Kitengo cha Ununuzi na Ugavi – Halmashauri ya Wilaya ya Longido
Karibu kwenye Kitengo cha Ununuzi na Ugavi (Procurement Management Unit - PMU) cha Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Kitengo hiki ni mhimili muhimu wa usimamizi wa rasilimali kupitia Ununuzi wa bidhaa, huduma, na kazi mbalimbali ndani ya Halmashauri. Kinafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma No. 5 ya mwaka 2023 kama inavosomeka katika kifungu cha 40(a)(b) Majukumu ya Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi "Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi (PMU) kitatekeleza shughuli zote za ununuzi kwa niaba ya taasisi nunuzi, ikiwa ni pamoja na kuandaa nyaraka, kuratibu michakato ya zabuni, na kusimamia mikataba ya manunuzi ya umma.”, kanuni zake, miongozo wa taratibu za Ununuzi na Ugavi katika vituo vya kutolea huduma, na miongozo ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma(PPRA) pamoja na usismaizi wa bodi ya wataalamu(PSPTB).
Uongozi wa Kitengo:
Kitengo hiki kinaongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Wilaya, ambaye anawajibika kuhakikisha taratibu zote za Ununuzi na Ugavi zinafanyika kwa mujibu wa sheria na maadili ya utumishi wa umma.
Majina Ya Watumishi Katika Kitengo Cha Ununuzi Na Ugavi katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.