• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

Kilimo, Mifugo na Uvuvi

1. UTANGULIZI

Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni miongoni mwa idara muhimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Idara hii ina jukumu la kuratibu, kusimamia, na kuendeleza sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuimarisha usalama wa chakula, kuinua kipato cha wananchi, na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Wilaya na Taifa kwa ujumla. Idara hutoa huduma za ugani kwa wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika sekta hizo.

2. DIRA YA IDARA

Kuwa kitovu cha maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi kinachotumia maarifa ya kisasa, rasilimali zinazopatikana, na ushirikiano wa wadau ili kuhakikisha usalama wa chakula, kipato cha wananchi na ustawi wa mazingira.

3. DHIMA YA IDARA

Kutoa huduma bora, za kitaalamu na zenye tija kwa wakulima, wafugaji na wavuvi wa Wilaya ya Longido kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia na rasilimali zilizopo kwa maendeleo endelevu.

4. MAJUKUMU YA IDARA

  • Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.
  • Kuratibu shughuli za uzalishaji wa mazao, mifugo na samaki.
  • Kuhamasisha matumizi ya teknolojia bora za kilimo na ufugaji.
  • Kusimamia uendeshaji wa mashamba darasa na vituo vya mafunzo kwa vitendo.
  • Kutoa elimu ya lishe bora ya mifugo na matumizi ya malisho bora pamoja na kuainisha maeneo ya malisho na kuyatolea hati miliki za kimila kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
  • Kuratibu huduma za chanjo na matibabu ya mifugo.
  • Kusimamia na kuratibu masoko ya mazao, mifugo na samaki.
  • Kuhamasisha uvuvi endelevu na ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa.
  • Kuratibu utekelezaji wa sera na miongozo ya serikali katika sekta hizi.

5. HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA

a) Sekta ya Kilimo

  • Ushauri wa kitaalamu kuhusu mbinu bora za kilimo ,na upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kwa wakati
  • Upatikanaji wa pembejeo za kilimo (mbegu bora, mbolea, viuatilifu n.k).
  • Mafunzo ya kilimo hai na kilimo cha kisasa.
  • Taarifa za masoko na bei za mazao.
  • Elimu ya kilimo cha umwagiliaji na uhifadhi wa mazao baada ya kuvuna.
  • Kujua afya ya udongo kwa kushirikiana na taasisi za utafiti hasa TARI na kutoa ushauri kwa wakulima na kufanya uchaguzi sahihi wa mazao sahihi ya kulima

b) Sekta ya Mifugo

  • Huduma za chanjo na matibabu ya mifugo.
  • Ushauri juu ya ufugaji bora na uboreshaji wa mifugo kwa kutumia madume bora(Sahiwal,Boran nk)
  • Elimu kuhusu lishe ya mifugo na malisho ya asili/malisho ya kisasa.
  • Utoaji wa vibali na usajili wa majosho na malambo.
  • Ujenzi wa miundombinu ya mifugo kama majosho, malambo, na minada pamoja na vibanio
  • Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa nyama na machinjio ili kupata zao bora la nyama kwa usalama wa walaji.

c) Sekta ya Uvuvi

  • Mafunzo ya uvuvi endelevu na ufugaji wa samaki.
  • Kutoa leseni na vibali vya uvuvi halali.
  • Elimu juu ya uhifadhi na usindikaji wa mazao ya uvuvi.
  • Kutoa huduma ya ushauri kuhusu uanzishaji wa mabwawa ya kufugia samaki.

d) Sekta ya Ushirika

 ni mfumo wa kiuchumi na kijamii unaojumuisha vyama vya ushirika vinavyolenga kuunganisha nguvu za wanachama hasa wakulima, wavuvi, wafugaji, na wajasiriamali ili kufanikisha maendeleo ya pamoja.

Hii ni sekta yenye historia ndefu, lakini hivi karibuni imeanza kupitia mageuzi makubwa ya kimfumo na kiteknolojia.

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido Sekta ya ushirika ina majukumu muhimu sana katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Majukumu yanayotekelezwa na Sekta ya Ushirika Ni kama ifuatavyo:

  • Kufanya uhaasishai na uanzishwai wa Vyama vya Ushirika,
  • Kufanya Ukaguzi na Usimamizi wa Vyam avya Ushirika,
  • Kutoa elimu na mafunzo kwa vyama vya Ushirika,
  •  Kuhifadhi na kuchambua takwimu za Vyama Vya Ushirika,
  • Kusimamia utekelezaji wa sera na sheria za ushirika,
  • Kutatua migogoro ndani ya vyama vya ushirika,
  • Kuviunganisha vyama vya ushirika na wabia wa biashara,

6. MIRADI YA MAENDELEO INAYOSIMAMIWA

  • Mradi wa upandaji wa mazao ya kimkakati kama mahindi, maharage, alizeti na viazi.
  • Mradi wa ujenzi na ukarabati wa majosho ya mifugo katika kata mbalimbali kama vile vijiji vya Eworendeke,Irkaswa,Engikaret, Olmog na sehemu zingine
  • Mradi wa ufugaji wa samaki kwenye mabwawa mfano kijiji cha Namanga,Longido nk
  • Mradi wa mashamba darasa ya kilimo bora cha kisasa mfano Namanga ,Longido
  • Mradi wa utoaji wa chanjo za mifugo Wilayani kote.
  • Mradi wa uanzishaji wa vikundi vya vijana na wanawake katika kilimo,Mifugo na uvuvi.
  • Kupunguza migogo kati ya wanyama pori dhidi ya wakulima na wafugaji kwa kuanzisha shamba darasa la mfano katika kijiji cha Tingatinga kwa kuanzisha mizinga ya nyuki.

7. MIKAKATI YA MWAKA 2025/2026

  • Kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
  • Kuboresha miundombinu ya mifugo na kilimo.
  • Kuwezesha wananchi kupitia vikundi vya uzalishaji na SACCOS.
  • Kupanua matumizi ya teknolojia za kisasa kwenye kilimo na ufugaji.
  • Kukuza ushirikiano na sekta binafsi katika masoko ya mazao na mifugo.
  • Kuhamasisha ufugaji wa samaki kama fursa ya kiuchumi kwa vijana.

8. WATUMISHI WA IDARA (Kwa mfano)

  • Mkuu wa Idara – Nestory Dagharo
  • Afisa Mifugo  –Dr.Safan Kagoma
  • Afisa Uvuvi  – 
  • Maafisa Ugani –

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 08, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA ( LINARUDIWA ) October 10, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA October 19, 2024
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA LONGIDO AWATAKIA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA KILA LAHERI KWENYE MITIHANI YAO

    September 09, 2025
  • HUDUMA ZA UPASUAJI ZAANZA RASMI KITUO CHA AFYA EWORENDEKE - LONGIDO

    September 06, 2025
  • HUDUMA ZA UPASUAJI ZAANZA RASMI KITUO CHA AFYA EWORENDEKE - LONGIDO

    September 06, 2025
  • RC ARUSHA ATOA WITO WA AMANI NA UTULIVU LONGIDO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

    September 04, 2025
  • View All

Video

PWC YATOA MSAADA KWA MASHIRIKA MADOGO LONGIDO KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.