NA MWANDISHI WETU, LONGIDO
Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) limedhamiria kuhakikisha linarejesha mazingira asilia ya Longido ambapo loe Oktoba 20, 2025 limeanza mafunzo ya siku mbili kwa Viongozi wa Dini na Viongozi wa Kimila wilayani Longido, yakilenga kuhamasisha jamii kuhusu sera na umuhimu wa utunzaji wa mazingira kupitia Mradi wa *Faith4Restoration*.
Mafunzo hayo yanayotekelezwa katika vijiji vya Orbomba, Kimokouwa na Eworendeke kwa lengo la kuongeza uelewa wa viongozi hao juu ya matumizi endelevu ya rasilimali asilia na maji, ni mwendelezo wa mafunzo yaliyoanza Juma lililopita yakijumuisha Viongozi wa Vijiji hivyo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kiongozi wa Mradi Prof. Noah Sitati alisema alisema Wilaya ya Longido imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya Tabianchi, hivyo ushawishi wa Viongozi hao ni muhimu katika kuhamasisha waumini wao kwenye masuala ya utunzaji mazingira.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka Ofisi ya WWF Arusha, Jane Shuma alisema kuwa Mradi unatekelezwa kwa miaka miwili ya majaribio na baadaye utafanyika katika Vijiji vingine.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.