UTANGULIZI:
Divisheni ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa divisheni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido, na ni kiungo muhimu kati ya Halmshauri na Jamii kwa kuratibu na kusimamia shughuli za kimaendeleo. Divisheni ya maendeleo ya jamii ina Jumla ya watumishi 15 ambapo wanaume 10 na wanawake 5 wanaotoa huduma kwa ngazi ya Wilaya na kata. Ambapo makao makuu ya willaya kuna watumishi 7 (me 3 ke 4) ngazi ya kata watumishi 8 (me 7 ke 1).
MALENGO LA DIVESHENI YA MAENDELEO YA JAMII
Kujenga uwezo wa jamii endelevu, kwa kuwezesha jamii katika kubaini mahitaji yao, kubuni, kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya kujiletea maendeleo kwa kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo kwa kujipatia na kujiongezea kipato kwa kuimarisha hali ya maisha ya jamii.
MUUNDO WA DIVISHENI
Divisheni ya maendeleo ya jamii inaongozwa na mkuu wa divisheni chini ya wasaidizi wawili ambao ni Mkuu wa sehemu ya masuala ya mtambuka na Mkuu wa sehemu ya mashirika yasiyo ya kiserikali. Chini ya sehemu mbili za Divisheni kuna Madawati tano ambayo ni:- Dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi na kupunguza umaskini,Dawati la uratibu wa kupambana na maambukizi ya ukimwi, Dawati la maendeleo ya jinsia na mtoto, dawati la ushirikishwaji wa jamii na dawati la uratibu, ufuatiliaji na usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGOS. Majukumu ya jumla ya Divisheni na madawati husika yameainishwa kama ifuatavyo:
MAJUKUMU YA JUMLA YA DIVISHENI YA MAENDELEO YA JAMII.
MAJUKUMU YA MADAWATI
HUDUMA ZITOLEWAZO NA DIVISHENI YA MAENDELEO YA JAMII.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.