HUDUMA ZA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI ZINAZOTOLEWA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO
Halmashauri ya Wilaya ya Longido kupitia Idara ya Elimu Msingi na Idara ya Elimu Sekondari inatekeleza jukumu muhimu la kutoa huduma bora za elimu kwa watoto na vijana wa Wilaya. Huduma hizi zinalenga kuinua kiwango cha elimu, kuongeza ufaulu, na kuhakikisha fursa sawa kwa wote. Zifuatazo ni huduma zinazotolewa:
Usajili wa Wanafunzi wa Darasa la Awali na la Kwanza
Kuandikisha watoto kuanzia miaka 4 kwa elimu ya awali na miaka 6 kwa darasa la kwanza kila mwaka.
Uendeshaji wa Shule za Msingi
Kusimamia shule za msingi za serikali na binafsi zenye kutoa elimu kuanzia darasa la awali hadi la saba.
Utoaji wa Elimu Bila Malipo
Serikali inatoa ruzuku ya elimu bila ada kwa wanafunzi wote wa shule za msingi (capitation grant).
Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu
Kujenga madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu, na mabweni ili kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Utoaji wa Chakula Mashuleni
Shule nyingi za msingi zinahamasishwa kuandaa na kutoa chakula ili kuboresha mahudhurio na ufaulu.
Utoaji wa Elimu Maalum
Kutoa huduma za elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Usambazaji wa Vitabu na Vifaa vya Kujifunzia
Kupokea na kusambaza vitabu kutoka serikalini kwa kila mwanafunzi kwa somo husika.
Ufuatiliaji na Tathmini ya Ufaulu
Kufanya ufuatiliaji wa maendeleo ya kitaaluma na nidhamu ya wanafunzi na walimu.
Maendeleo ya Walimu
Kutoa mafunzo kazini, warsha na semina mbalimbali kwa walimu ili kuongeza ufanisi.
Usajili wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza
Kuandikisha wanafunzi wanaofaulu mtihani wa darasa la saba kujiunga na kidato cha kwanza.
Uendeshaji wa Shule za Sekondari
Kusimamia shule za sekondari za kutwa na bweni, za serikali na binafsi.
Elimu Bila Malipo kwa Kidato cha I-IV
Kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za sekondari kupitia ruzuku ya serikali.
Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu
Kujenga madarasa, maabara, maktaba, mabweni na nyumba za walimu.
Utoaji wa Elimu kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum
Kuhakikisha shule zinakuwa jumuishi na zinawawezesha wanafunzi wote kupata elimu bila ubaguzi.
Mafunzo Endelevu kwa Walimu wa Sekondari
Kuendeleza uwezo wa walimu kupitia mafunzo kazini na warsha.
Usambazaji wa Vitabu vya Kiada na Zana za Maabara
Kusambaza vitabu vya mtaala mpya na vifaa vya kufundishia hasa kwa masomo ya sayansi.
Ufuatiliaji wa Taaluma na Nidhamu
Kufanya ziara shuleni kwa ajili ya ufuatiliaji wa ufaulu na mwenendo wa wanafunzi na walimu.
Elimu ya Kujitegemea na Mafunzo ya Ufundi
Kutoa elimu inayowaandaa wanafunzi kwa stadi za maisha kupitia masomo ya kilimo, biashara, na ufundi.
Ushirikiano na Wadau
Kufanya kazi kwa karibu na wazazi, jamii na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuboresha elimu.
Halmashauri ya Wilaya ya Longido imeendelea kujitahidi kuboresha elimu kwa kuhakikisha watoto wote wanapata haki yao ya msingi ya kujifunza katika mazingira salama na rafiki kwa mtoto.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.