Na HAPPINESS NSELU,
Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido imefanya kikao chake cha robo ya kwanza cha mwaka wa fedha katika ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo, kikao ambacho kimeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido,Bw. Nassoro Shemzigwa.

Kikao hicho kimekutanisha wajumbe kutoka idara mbalimbali za Halmashauri zikiwemo afya, elimu, kilimo na maendeleo ya jamii pamoja na wadau wa lishe kutoka taasisi nyingine.


Lengo la kikao lilikuwa ni kujadili utekelezaji wa shughuli za lishe katika robo iliyopita, kuainisha mafanikio, changamoto na kuweka mikakati ya kuboresha hali ya lishe katika jamii.


Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: +255 272 970 793/ 94
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.