UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA
Halmashauri ya wilaya ya Longido imepokea pesa toka serikali ya awamu ya tano kiasi cha Tsh. Bilioni moja na nusu(1.5b) kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya. Halmashauri ya Longido haikuwai kuwa na hospitali ya Wilaya mpaka mwaka huu ilipopatiwa pesa na serikali ya awamu ya tano na ujenzi kuanza mara moja,ujenzi huu bado unaendelea.
Ujenzi huo utakuwa na majengo ya saba ambayo ni
JENGO LA WAGONJWA WA NJE.(OPD)
Jengo la wagonjwa wa nje kama linavyoonekana hapo juu ni kwamba wapo katika hatua ya mwisho ya kupanga mawe tayari kabisa kwa kuweka jamvi.
JENGO LA UTAWALA
Jengo la utawala kama linavyo onekana hapo juu tayari msingi kwa sasa wanweka kitu kinachoitwa colums ,baada ya hapo wanweka nguzo na kumwaga zege.
JENGO LA MIONZI(X- RAY)
Jengo la mionzi tayari msingi umeshachimbwa wako tayari kwa hatua nyingi ya kumwaga zege.
JENGO LA MAABARA
Jengo la maabara tayari msingi ni kwamba udongo ndio imnazawazishw ili mawe yapangwe.
JENGO LA KUFULIA(LAUNDRY)
Jengo la kufulia kama linavyo onekana hapo juu tayari mawe yamepangwa saiv ni kumwaga jamvi tuu.
JENGO LA MAMA NA MTOTO
Jengo la mama na mtoto kama inavoonekana hapo juu tayari mawe yameshapangwa na tayaripia kwa kumwaga jamvi.
JENGO LA MADAWA (PHARMACY)
Jengo la madawa kama inavyoonekana hapo juu ni kwamba ndio linanyuliwa sasa.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM