Mkuu wa idara ya Mifugo na Uvuvi. Ndg.Nestrory Dagharo
Namba ya simu 0782749201
Kiasi cha asilimia 95 ya eneo la Wilaya ya Longido linatumika kwa ufugaji na wanyamapori. Kati ya hekta 778,200 za Wilaya eneo la malisho ni hekta 639235 (tazama jedwali 1). Wilaya ina Ng’ombe 216,575 wa
nyama na ng’ombe wa maziwa 273, Mbuzi wa nyama 399,754, kondoo 301,211, Kuku 15,666, Punda 15,339, Nguruwe 153 na Mbwa 15,012 na Ngamia 180.
Matumizi |
Eneo (KM za Mraba) |
Hekta |
% |
Eneo linalotumika kwa Kilimo
|
292.23 |
29223 |
3.76 |
Eneo la Malisho
|
6392.35 |
639235 |
82.14 |
Eneo linalofaa kwa Kilimo
|
731.75 |
73175 |
9.4 |
Misitu
|
365.75 |
36575 |
4.7 |
Jumla Eneo la Wilaya
|
7,782 |
778,200 |
100 |
MIUNDOMBINU YA MIFUGO
Wilaya ina miundombinu mbali mbali kwa matumizi ya mifugo ikiwa ni pamoja na majosho, mabwawa, malambo, vibanio, mabirika, minada na machinjio. Hali ya miundombinu ya mifugo ni kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapa chini;
Jedwali 2: HALI HALISI YA MIUNDO MBINU YA MIFUGO
AINA
|
MAHITAJI
|
IDADI ILIYOPO
|
MAZIMA/IMARA
|
MABOVU
|
UPUNGUFU
|
Majosho
|
64
|
24
|
11
|
12
|
41
|
Mabwawa
|
72
|
9
|
8
|
-
|
63
|
Malambo
|
120
|
25
|
25
|
-
|
95
|
Vibanio
|
96
|
45
|
45
|
-
|
51
|
Mabirika
|
96
|
48
|
48
|
-
|
48
|
Machinjio
|
2
|
2
|
2
|
-
|
-
|
Minada
|
11
|
11
|
2
|
9
|
9
|
1.2 HALI HALISI YA WATUMISHI WA UGANI MIFUGO
Idara ya Mifugo na Uvuvi ina jumla ya watumishi 21 kati ya 64 wanaohitajika, upungufu 43 wanaohitajika kulingana na huduma zinazohitajika katika kata 18 na vijiji 49 vya Wilaya. Aidha jumla ya Maafisa Ugani wa Mifugo 14 wapo ngazi ya Kata, kati yao 11 wana usafiri wa pikipiki.
Katika kuboresha/kuimarisha upatikanaji wa huduma za ugani Wilaya imewapatia Maafisa Ugani 12 pikipiki na magari 2 yapo Makao Makuu ili kuimarisha utendaji kazi katika maeneo yao. Pikipiki hizo zinasaidia Maafisa Ugani kuwafikia wafugaji na kuwafundisha mbinu za ufugaji bora. Hii imesaidia kuboresha Mifugo na kuongeza uzalishaji.
1.3 HALI YA HEWA
Wilaya ya longido ni moja ya Wilaya iliyopo kwenye nyanda kame hapa nchini. Wilaya inapata wastani wa mvua kiasi cha 500mm maeneo ya ukanda wa chini na 900mm maeneo ya ukanda wa juu kwa mwaka, kama kuna mtawanyiko mzuri wa mvua. Wakati mwingine hupata wastani wa 500mm kwa mwaka wenye uhaba wa mvua.
1.4 FURSA ZILIZOPO
Wilaya ina fursa ya kuwekeza kwenye sekta ya Mifugo hasa biashara ya mifugo na mazao yake. Mifugo wa Longido hasa ng’ombe, mbuzi na kondoo wameboreshwa kwa asilimia 65 hivyo kuna fursa kwenye uwekezaji kwenye mifugo na mazao yake.
Wilaya ina eneo kubwa la nyanda za malisho linaloweza kuendelezwa lenye ukubwa wa kilometa za mraba 6392.35 eneo ambalo likipata fedha za kuwekeza katika kukarabati/kuboresha nyanda za malisho itasaidia mifugo kupata malisho ya kutosha kwa mwaka mzima.
Wilaya ikishirikiana na wadau mbali mbali imekuwa na harakati endelevu za kupambana na magonjwa mbali mbali ya mifugo ikiwemo magonjwa ya mlipuko.
HUDUMA
|
UGONJWA
|
AINA YA MIFUGO ILIYOCHANJWA
|
IDADI YA MIFUGO ILIYOCHANJWA
|
Chanjo
|
Upele wa Ngozi kwa ng’ombe
|
Ng’ombe
|
129,967
|
Chanjo
|
Ndigana Kali
|
Ng’ombe
|
88,423
|
Chanjo
|
Homa ya Mapafu kwa ng’ombe
|
Ng’ombe
|
123,987
|
Chanjo
|
Kichaa cha mbwa
|
Mbwa
|
4,178
|
Chanjo
|
Kideri
|
Kuku
|
8,098
|
Elimu ya ufugaji bora unaozingatia utaalamu imetolewa kwa vikundi 50 vya wafugaji ambavyo 15 ni vya unenepeshaji wa ng’ombe katika Kata 8 na jumla ya madume 360 yalinenepeshwa na kuuzwa, vikundi 64 ni vya Wanawake kwa ajili ya ufugaji wa bora wa kuku chini ya mradi wa maisha bora ili kuwawezesha kuinua pato lao kutokana na mifugo. Aidha kupitia mradi wa Maisha Bora unaofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji vijiji 8 vyenye jumla ya vitongoji 35 vimenufaika na kila kikundi kitapata madume bora kwa vikundi vya wanaume na wanawake watapata mbuzi na kuku.
Wananchi wa Longido bado wanaendelea kuishukuru Serikali kwa kupata mradi wa Mifugo ya Kifuta Machozi ili kukabiliana na janga la ukame lililotokea mwaka 2008/2009. Katika mpango wa kutoa Mifugo ya Kifuta Machozi, Wilaya iliidhinishiwa jumla ya Tshs. 5,704,000,000/= kwa ajili ya ununuzi wa Ng’ombe 11,408 na Mbuzi 14,260 kwa ajili ya kaya 2,852 zilizopoteza mifugo yao yote. Hadi 2016, jumla Tshs. 2,989,000,000 zilikwishatolewa na kutumika katika ununuzi wa Ng’ombe na mbuzi ambapo ng’ombe 6,805 na mbuzi 3,340 tayari waligawiwa kwa kaya 1,701. Mradi huu umesaidia sana familia zilizopoteza mifugo yote na kuweza kurudi tena kwenye shughuli zao za kiuchumi za ufugaji.
UBORESHAJI WA MIFUGO
Katika jitihada za kuboresha mifugo wa asili Wilaya kwa kushirikiana na wadau hasa mashirika yasiyo ya Kiserikali CORDS, PWC imewanunulia Wafugaji madume bora ya ng’ombe 65, mbuzi na kondoo 50. Aidha Wafugaji wenye uwezo wanaendelea kujinunulia wenyewe madume bora.
Mbuzi walioboreshwa (Aina ya Isiolo) wakiwa Malisho
Kondoo Walioboreshwa kwa Madume Bora aina ya Black Head Persian
Vijijji vyote 49 vya Wilaya vina mpango wa matumizi bora ya ardhi na maeneo ya malisho yameainishwa kwa kila kijiji. Maeneo ya hifadhi ya malisho kiasili yameainishwa na kutunzwa kulingana na taratibu za kimila.
3.0 CHANGAMOTO
4.0 MIKAKATI /UTATUZI WA CHANGAMOTO
Wilaya ina mikakati/mipango mbali mbali kuendeleza sekta ya mifugo kama ifuatavyo:-
Kuomba kwenye bajeti ya kila mwaka kuajiriwa Maafisa Ugani Mifugo.
Kuhamasisha wenye mifugo wengi kuwa na malambo kwenye maeneo yao.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM