HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI
IDARA YA UTUMISHI NA UTAWALA
MUUNDO WA HALMASHAURI NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA OFISI YA UTUMISHI
MAELEZO MAFUPI WILAYA:
Halmashauri ya Wilaya ya Longido ni mojawapo ya Wilaya saba (6) zilizopo Mkoa wa Arusha ambapo nyingine ni Halamashauri ya Wilaya ya Arusha, Karatu, Meru, Monduli na Ngorongoro.
ENEO
Wilaya ya Longido ina eneo la Kilomita za Mraba __________ ambayo ni sawa na ______ya eneo lote la Mkoa wa Arusha.
IDADI YA WATU
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2012 Wilaya ya Longido ina jumla ya wakazi 123153 kwa Sensa ya 2012 142597 kwa makadirio ya 2017 ambapo wanawake ni _________na wanaume ni ______________Makabila makubwa ni Wamasai kwa asilimia 90.
IDADI YA WATUMISHI
Halmashauri ya Wilaya ya Longido hadi kufikia Mwezi June 2017 ilikuwa na juml ya watumishi 1,117.
UTAWALA
Wilaya ina jimbo moja la Uchaguzi, Tarafa Nne (4), Kata Kumi na Nane (18),Vijiji arobaini na tisa (49) na Vitongoji Mia moja na sabini na tano (175).
UONGOZI
Wilaya ina Mbunge mmoja (1) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Madiwani kumi na nane (18) wa kuchaguliwa na Madiwani sita (6) wa kuteuliwa (Viti Maalum)
MUUNDO WA HALMASHAURI
Baraza la Madiwani; Chombo Kikuu cha kufanya maamuzi yote yahusuyo mambo mbalimbali ya Halmashauri
Kamati za Kudumu za Halmashauri; Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango,Huduma za Jamii (Elimu, Afya na Maji), Uchumi, Ujenzi na Mazingira na Kamati Shirikishi ya Kudhibiti UKIMWI.
Bodi za Halmashauri; Bodi ya Ajira na Bodi ya Zabuni
Mkurugenzi Mtendaji, na Vitengo vinavyoripoti moja kwa moja;Kitengo cha Sheria,Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Uchaguzi na Ugavi.
Idara za Halmashauri; Idara ya Utumishi na Utawala,Idara ya Fedha na Biashara, Afya, Mipango,takwimu na Ufuatiliaji,Maendeleo ya Jamii,Kilimo na Umwagiliaji, Maji na Udhibiti takangumu, Usafi na Mazingira,Ujenzi na Zimamoto, Ardhi na Maliasili, Mifugo na Uvuvi Elimu Msingi na Ulimu Sekondari.
JUKUMU LA IDARA:
Jukumu la Msingi la Idara ya Utumishi na Utawala ni kusimamia matumizi bora yenye ufanisi ya Rasilimali watu katika kutoa huduma kwa kuhakikisha Rasilimali watu inatumiwa kutekeleza shughuli za Halmashauri kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo.
Kazi zinazofanywa na Idara.
Ili kutimiza jukumu la msingi lililotajwa hapo juu Idara inatekekeza shughuli zifuatazo:-
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM