KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ni moja ya Kamati za kudumu za Halmashauri na inaundwa kwa kushirkisha Wenyeviti wa Kamati za Kudumu na hukutana mara moja kila mwezi na moja ya majukumu yake ya Msingi ni pamoja na kusimamia na kudhibiti ukusanyaji wa mapato na matumizi ya mali za Halmashauri kupitia Vikao vyake. Majukumu mengine ni;
Kuweka mikakati na kupendekeza uongezaji wa mapato
Kuwasilisha mapendekezo ya bajeti na Mpango wa Maendeleo wa Halmashauri ili kuidhinishwa na Halmashauri
Kusimamia utunzaji wa fedha ikiwa ni pamoja na kufuta madeni, kuhakiki mali za Halmashauri, kuomba vibali maalum kwa matumizi yanayohitaji kibali cha Waziri mwenye dhamana
Kufikiria na kupendekeza mabadiliko ya viwango vya kodi, ada na ushuru mbalimbali vinavyotolewa na Halmashauri
Kushughulikia orodha ya wadaiwa wote itakayowasilishwa kwenye Kamati na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua
Kujadili na kupendekeza masuala yote yanayohusu maslahi ya jumla ya Watumishi ikiwa ni pamoja na kuthibitisha Watumishi kazini, mikopo, nyumba, usafiri, matibabu, rambirambi, masomo na motisha nyinginezo
Kupokea na kuzingatia mapendekezo ya kubadili matumizi ya mafungu ya fedha yaliyopo kwenye makisio (reallocation) na kuyawasilisha kwenye Halmashauri
Kuratibu mapendekezo kutoka kwenye Kamati nyingine kuhusu matumizi ya kawaida na miradi na kuyawasilisha kwenye Halmashauri
Kufikiria na kupendekeza kwenye Halmashauri kuhusu Mikopo yote ya Halmashauri
Kutoa mapendekezo ya vitega Uchumi kwa madhumuni ya kuongeza mapato kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290
Kupokea na kujadili Taarifa za Wakaguzi wa Fedha na mali za Halmashauri na kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na maelekezo na maoni ya Wakaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura ya 290
Kupokea na kudhibiti matumizi ya fedha za Halmashauri kwa kuzingatia Taratibu zilizowekwa na Waziri na nyingine zitakazowekwa na Halmashauri
Kupitia marekebisho yote yaliyopendekezwa hususan kuhusu taratibu za fedha ikiwa ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara yanayohusu thamani ya fedha ambapo Kanuni mbalimbali za Manunuzi ya mali na Vifaa hutumika.
Kushughulikia tofauti ya Mapato na Matumizi kwenye Bajeti na kupendekeza hatua stahili za kuchukua
Kupokea na kujadili Taarifa za Fedha kila mwezi na Robo mwaka
Kushughulikia Sera kuhusu kukopa na Uwekezaji
Kubuni na kupendekeza mpango wa kuanzisha na kuendeleza uhusiano na Halmashauri nyingine
Kurekebisha na kusimamia makusanyo na matumizi ya Mapato ya Vijiji kwa mujibu wa Sheria Sura ya 287
Kuteua Wakaguzi wa Fedha/Mali za Serikali za Vijiji kwa mujibu wa Sheria, Sura ya 290
WAJUMBE WA KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO KWA MWAKA WA FEDHA 2018/2019
NA
|
JINA |
KATA |
CHAMA |
1
|
MHE. SABORE K. MOLLOIMET
|
M/KITI WA HALMASHAURI - MWENYEKITI
|
CCM
|
2
|
MHE. ESUPAT K. NGULUPA
|
MAKAMU MWENYEKITI – VITI MAALUM
|
CCM
|
3
|
MHE. ALAIS MUSHAO
|
M/KITI WA KAMATI YA ELIMU, AFYA & MAJI
|
CCM
|
4
|
MHE. PETER LEKANETI
|
M/KITI WA KAMATI YA UCHUMI, UJENZI & MAZINGIRA
|
CCM
|
5
|
MHE. PETER NDEREKO
|
M/KITI WA KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
|
CCM
|
6
|
MHE. DR STEPHEN KIRUSWA
|
MBUNGE
|
CCM
|
7
|
MHE. MOTIKA KASOSI
|
ORBOMBA
|
CCM
|
8
|
MHE. SARA OLTETIA
|
VITI MAALUM – MUNDARARA
|
CCM
|
9
|
MHE. JOPHA KAKANYI
|
VITI MAALUM – ENGARENAIBOR
|
CCM
|
10
|
MHE. UPENDO MTAGWA
|
VITI MAALUM – LONGIDO
|
CHADEMA
|
11
|
MHE. TIMOTHEO MONYORIT
|
KETUMBEINE
|
CCM
|
12
|
MHE. SIMON OITESOI
|
GELAI LUMBWA
|
CCM
|
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM