Kitengo cha uchaguzi hujishughulisha na usimamizi wa chaguzi za Kidemokrasia katika jamii.Demokrasia watu mamlaka ,huruhusu jamii kujichagulia viongozi wanaowataka kwa masilahi ya jamii.Viongozi wanaochaguliwa ,hulinda,hutetea,hubuni na kufanikisha matakwa na matazamio ya jamii husika na hapo ndipo utawala bora unapokuwa hai.
Kitengo cha uchaguzi husimamia jamii kufanya maamuzi yao kwa mujibu wa katiba katika kuwapata viongozi wanaowataka kuanzia ngazi ya vitongoji,vijiji majimbo na nchi kwa njia ya kupiga kura.Kitengo cha uchaguzi hushirikiana na tume ya taifa ya uchaguzi kufanya michakato mbalimbali katika kutekeleza hitaji la jamii la kuwapata viongozi bora kwa amani na utulivu wenye kuleta,kulinda na kuendeleza maendeleo ya jamii ,kiuchumi,kiutamaduni ,kijamii na kisiasa.
Kitengo hutegemea mtaji wa wapiga kura na wapigiwa kura katika uchaguzi wowote ule,uchaguzi mkuu na mdogo HIVYO; DEMOKRASIA → UCHAGUZI HURU→ UONGOZI BORA → MAENDELEO ENDELEVU → MAISHA BORA → UPENDO NA UMOJA DUNIANI.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM