Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa J K Nyerere Tarehe 05/04/2024.
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mheshimiwa Simon Oitesoi amewataka wawekezaji hao kutoa Elimu ya kutosha kwa wajumbe ili kuwasaidia kuwa na Elimu thabiti kabla hawajakaa mezani na kusaini mkataba huo.
"Kwa kuwa biashara hii kwetu ni mpya niwaombe mtengeneza mazingira mazuri ya sisi kutoka ili tukajifunze kwa waliofanya, na sisi tuwe na uelewa wa pamoja kwa sababu kwetu katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido ni mpya tumesikia maeneo mengine wanafanya biaahara kama hii ila sio kwenye udongo sasa ili tuwe na uelewa mzuri tukajifunze kwa waliofanya kwanza "Alisema Mhe Oitesoi.
Akiwasilisha Rasimu ya Mkataba huo Mwanasheria wa Halmashauri Ndugu Dominic Ruhamvya amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa kwa kuwa bado ni Rasimu imeletwa mezani ili ijadiliwe na hatimae baraza liamue na kufanya maamuzi yaliyo sahihi juu ya Matumizi bora na sahihi ya Ardhi hasa kwenye maeneo ya Malisho ambapo Longido inalisha wanayama wa kufuga na Wanyama wasiofungwa.
Vile vile Bwana Ruhamvya amewaleza wajumbe kuwa Mradi huu haukusudii tu kukuza uendelevu wa mazingira bali pia kuimarisha uhamishaji wa teknolojia na maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii kwa kuzalisha na kugawana mapato yanayotokana ma mauzo ya viwango vya kaboni ambayo yanaweza kutumika kutoa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na mazingira safi, yenye afya na endelevu na kuboreshwa kwa huduma za kijamii.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Ndugu Nasorro Shemzigwa amesema kwamba iwapo tutafikia muafaka juu ya usainishwaji wa Mkataba huu wa biashara ya hewa ya Ukaa mbali tu na kupata mapato, pia itasaidia sana kwenye utunzaji wa mazingira yetu, kwetu sis, kwa mifugo na wanyama wetu.
Sambamba na kuiomba Kampuni juu ya utoaji wa Elimu ya kutosha kw a wajumbe, pia amewaasa wajumbe hao kutoa Elimu ya kutosha kwa jamii juu ya uwekezaji huu wa Hewa ya ukaa waelezwe kuhusu faida zitakazo patikana kutokana na utunzaji wa mazingira.
Tafadhali niwaombe wawekezaji watupeleke darasani tukajifunze tujua kwa wenzetu waliokwisha anza kufanya biashara hii iwe ndani ama nje ya nchi ya Tanzania. "Alisema Mheshimiwa Abel Njipai Diwani wa Noondoto.
Rasimu ya Mkataba huu imeainisha madhumuni ya Mkataba, masharti ya awali tarehs na muda, mgawanyo wa gharama na faida, taarifa za fedha na matumizi y a faida, Msamaha, Mkataba mzima, Uhalali, Taarifa, Sheria inayotumika, Ukomo wa Mkataba, majanga ya Asili,pamoja na Usuluhishi wa migogoro.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM