Akizindua zoezi Mheshimiwa Ng'umbi ameitaka jamii kuto kupuuza kwa baadhi ya magonjwa na badala yake kuwa makini na magonjwa yote yanayoambukiza na yasio ambukiza.
Zoezi hili la umezeshwaji wa dawa za magonjwa ya Minyoo ya tumbo na kichocho linataraji kuwafikia watoto wasiopungua elfu 35,609 wa Wilaya ya Longido Kuanzia miaka mitano hadi 14. Zoezi linataraji kufanyika katika shule 70 za Wilaya ya Longido na vituo teule 9.
Mheshimiwa Ng'umbi amefungua zoezi hili leo tarehe 29/02 /2024 katika shule ya Msingi Longido ambapo watoto zaidi ya elfu elfu 1, 264 katika shule hiyo wamepatiwa dawa hizo kwa ajili ya Minyoo ya tumbo na Kichocho.
Mheshimiwa Ng'umbi amewataka wawezeshaji wa zoezi hilo la ugawaji wa dawa kuwafikia watoto wote waliopo katika kata zote na vitungoji vyake vilivyopo Wilayani Longido"Niwaombe wawezeshaji na waendashaji wa zoezi hili kuwafikia watoto wote hata wale waliopo majumbani ambao hawajaenda shule ili na wao wapatiwe tiba hii ya kujikinga na magonjwa hayo"Alisema Mheshimiwa Ng'umbi.
Zoezi la umezeshwaji wa dawa hizi za Kinga tiba ni zoezi la siku mbili Ambapo linataraji kufika ukomo tarehe 29/02/2024.
Jamii inaaswa kuhakikisha watoto wote wanapatiwa dawa hizo kwani hazina madhara yoyote kwa watoto badala yake ni Kinga ya magonjwa hayo ya Minyoo ya tumbo na Kichocho.
Nae Daktari Mathew Majani ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau Kutoka RTI kwa kuwezesha upatikanaji wa dawa hizo za kinga Tiba.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM