Leo Tarehe 10-08-2021Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe Nurdin Babu amefungua mafunzo ya kuibua kaya maskini kwa wawezeshaji ngazi ya Vijiji kwenye mpango wa TASAF II awamu ya III unaotarajia kufanyika baada ya mafunzo hayo kwa Vijiji ambavyo havikuwepo kwenye mpango huo wa kunusuru kaya maskini Mafunzo hayo pia yanayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri umehudhuriwa na Madiwani kutoka kata husika, kamati ya ulinzi na usalama wilaya na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe Nurdini Babu, wakati wa akifungua Mafunzo iliyohusisha wawezeshaji, watakaokwenda kuzibaini kaya masikini ambazo zitaingia kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini mpango wa pili wa TASAF awamu ya tatu, pamoja na waheshimiwa madiwani, timu ya menejimenti ya halmashauri hiyo, semina iliyofanyika kwenye viwanja vya halmashauri ya Longido.
Mkuu wa wilaya Mhe.Nurdin Babu aliwataka wawezeshaji watakaoenda kufanya kazi ya kuibua Kaya masikini kupitia mradi wa kipindi cha pili TASAF awamu ya III, wametakiwa kufanyakazi hiyo kwa weledi na uaminifu mkubwa, ili kuwapata walengwa wenye sifa na vigezo vilivyoaainishwa, kaya ambazo zinakabiliwa na lindi la umasikini uliokithiri, ili kufikia malengo ya serikali ya kupambana na adui umasikini kwa maendeelo ya Taifa la Tanzania.
Mhe Nurdini Babu, amewasisitiza kuwa, wawekezaji hao wameaminiwa na serikali na kuwakabidhi jukumu la kwenda vijijini kubaini kaya masikini zitakazoingizwa kwenye mpango wa ruzuku za TASAF, hivyo wanao wajibu wa katumia fursa vizuri na kwa uadilifu mkubwa, wakiweka uzalendo mbele kwa kufuata vigezo na taratibu zilizowekwa na serikali kupitia TASAF vya kubaini kaya hizo, huku akiwataka waheshimiwa madiwani kutumia majukwaa yao, kuwaeleimisha wananchi sifa na wajibu wa walengo katika mradi huo uliotolewa na serikali katika maeneo yao.
Aidha, Mkuu wa Wilaya, amefafanua kuwa, lengo la kuendeleza mradi huu ambao tayari, ulifanya vizuri katika awamu ya kwanza, serikali imeona ni vyema kuendelea na mradi huo kwa awamu ya pili, na kuzifikia kaya masikini na zenye sifa katika vijiji vyote vya halamshauri na nchi nzima, lengo likiwa ni kuziwezesha kaya hizo, kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa za kujiongezea kipato, huduma za jamii na kuwekeza katika kuendeleza watoto, pamoja na kuondokana na lindi za umasikini uliokithiri kwa maendeleo ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa halmshauri ya Longido, Mhe. Simion Oitesoi, amesema kuwa, zoezi la kubaini kaya masikini, ni zoezi la msingi mno, katika halmashauri ya Longido, kutokana na ukweli kwamba kaya nyingi hususani kwenye maeneo ya vijijini ziko katika hali mbaya kiuchumi, zikikabiliwa na changamoto za kuendesha maisha na kushindwa kumudu hata kupata mlo mmoja kwa siku na kuwataka waheshimiwa madiwani wote kuhakikisha wanahamasisha wananchi kupitia mikutano mbalimbali inayofanyika kwenye maeneo yao ili wananchi wajitokeze kwa wingi ili zoezi lifanikiwe kama ilivyokusudiwa pia kuwasaidia wananchi kuibua miradi itakayokuwa na tija kwa jamii zetu.
Mhe Simion Oitesoi alisisitiza kuwa "Nina wasihi wawezeshaji wote, tambueni kuwa kazi hii mmepewa ni dhamana ya maisha ya watu, serikali imewaamini, hakikisheni mnaifanya kwa uadilifu na kwa kuzingatia haki, kila mmoja wenu ahakikishe anabaini na kuandikisha kaya zenye sifa ya umasikini uliokithiri na si vinginevyo, kaya ambazo zina uhitaji mkubwa wa kusaidiwa na serikali ili waweze kujikwamua lakini pia waheshimiwa madiwani tambueni mna wajibu wa kuwaelimisha wananchi wenu, kuifahamu vizuri TASAF na mradi huu wa kaya masikini pamoja na wajibu wa walengwa katika mradi huo wa TASAF, tumieni mafunzo haya kuwaelimisha wananchi wenu ili kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima".
"Ninaipongeza serikali ya awamu ya sita, kwa kuona umuhimu wa kuzifikia kaya masikini kwenye vijiji vyote vya halmashauri, hali ambayo licha ya kuwezesha kaya hizo kujimudu kiuchumi lakini itapunguza malalamiko yaliyokuwepo kwa serikali, kupitia mafunzo haya, mimi na madiwani wenzangu, tuna jukumu lamkuelimisha wananchi wetu, waufahamu mradi huu wa TASAF, sifa za kaya zinazohitajika pamoja na wajibu wa kaya masikini katika miradi hiyo ya TASAF" Amefafanua Mheshimiwa Simon.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TASAF Makao Makuu, Bi Nuru mwezeshaji ngazi ya kitaifa, ameweka wazi sifa za walengwa watakoandikishwa katika kipindi cha pili cha mradi wa TASAF awamu ya tatu kaya zenye kipato cha chini sana na si cha uhakika,kaya ambazo haziwezi kumudu milo mitatu kwa siku, kaya inayoishi kwenye makazi duni, kaya ambayo inawatoto lakini hawaendi shule na kaya ambayo inawatoto wengi hivyo kushindwa kumudu gharama za mahitaji.
Aidha Bi Nuru amefafanua kuwa, licha ya kuwa mradi huu,utatoa ruzuku ya fedha kwa kaya masikini lakini pia kutakuwa na miradi ya kutoa ajira ya muda kwa walengwa, ambapo kaya itataikiwa kuandikisha watu wawili kufanya ajira za muda, lengo likiwa ni kuongezea kaya kipato pamoja na kuwaongezea ujuzi kupitia kazi husika.
Hata hivyo wawekezaji hao 28, wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa umahiri na umakini mkubwa huku wakiweka mbele maslahi ya Taifa, kupitia weledi na uzalendo, kwa maendeleo ya kaya masikini ili waweze kutumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini uliokithiri.
Awali, katika kipindi cha pili cha mradi wa TASAF awamu ya pili, ulizinduliwa rasmi mwaka 2020 mpaka 2023, na unategemea kutumia kiasi cha shilingi trilioni 2.3 na kutekelezwa katika halmashauri 184 za Tanzanzia Bara na visiwani, na kufika jumla ya kaya milioni milioni moja na laki nne na nusu, zenye jumla ya watu milioni saba kote nchini, huku halmashauri ya Longido, ukitegemea kutekelezwa katika kata 18 na vijiji 56.
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM