Shughuli za Uwindaji katika Wilaya ya Longido
Wilaya ya Longido ni eneo la Pori tengefu la Wanyamapori (Game Controlled Area) ambapo takribani asilimia 95 ya eneo lote la wilaya limehifadhiwa kwa ajili ya shughuli za Uvunaji na usio wa Uvunaji wa Wanyamapori (Consumptive and Non Consumptive Utilization). Eneo hili lina ukubwa wa takribani kilomita za mraba 7,000.
Ndani ya wilaya, kuna vitalu saba vya uwindaji vinavyotumika kwajili ya shughuli za Utalii wa uwindaji wa nyara (trophy hunting).
S/N
|
JINA LA KITALU
|
KAMPUNI INAYOMILIKA
|
1
|
LAKE NATRON G,C.A NORTH
|
ADAM CLEMENTS SAFARIS
|
2
|
LAKE NATRON G.C.A SOUTH
|
ROBIN HURT HUNTING SAFARIS
|
3
|
LAKE NATRON G.C.A WEST
|
KILOMBERO NORTH HUNTING SAFARIS
|
4
|
LAKE NATRON G.C.A EAST
|
GREENMILE HUNTING SAFARIS
|
5
|
LONGIDO G.C.A
|
MICHEL MANTHEAKIS SAFARIS
|
6
|
MONDULI JUU OPEN AREA
|
TANZANIA BIG GAME SAFARIS
|
7
|
ENGASURAI WMA ENDUIMET
|
WEMBERE HUNTING SAFARIS
|
Wilaya ina takribani spishi 40 za wanyamapori pamoja na aina nyingi za ndege, zikiwemo ndege wahamiaji aina ya flamingo ambao Ziwa Natron ndilo eneo pekee duniani wanalozaliana.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Ikolojia wa mwaka 1980, idadi ya wanyamapori katika wilaya inakadiriwa kufikia wanyama 100,000, huku msongamano wao ukiwa wastani wa 6.7 kwa kila kilomita ya mraba (kwa mujibu wa takwimu za mwaka 1984).
Kwa Mawasiliana na Msaada zaidi fika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Longido
au piga simu namba
0784889889 Afisa Wanyamapori
0787115234 Afisa Utalii
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.