Magonjwa ya Utapiamlo yameendelea kupungua kwa asilimia moja (1%) kutoka 1.5% hadi 1.4% katika kipindi cha Januari – Machi hayo yamesemwa leo tarehe 14/05/2019 katika kikao cha Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa robo ya tatu(Januari mpaka Machi) 2019 katika ukumbi wa Halmashauri na kuhudhuliwa na wajumbe wa kamati hiyo.
Tathimini iliyofanyika katika robo hiyo ya tatu inaonesha kiwango cha utapiamlo kimepungua kwa asilimia 1% kutoka 1.5% hadi 1.4% . Kupungua huko kumeambatana na utoaji wa Elimu inayotolewa na kitengo cha Elimu kwa Wazazi na Walezi juu ya umuhimu wa Vitamin A na dawa za minyoo kwa watoto, kuwapeleka cliniki kwa kuzingatia tarehe walizopangiwa kurudi kwa ajili ya kupima maendeleo ya watoto.
Vilevile tathmini iliyofanyika inaonesha kuwa watoa huduma ngazi ya jamii kwa kushirikiana na wahudumu wa Afya kwenye vituo vya kutolea huduma walitoa elimu ya umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzo na hata pale mtoto atakapokuwa ameanza kupewa vyakula mpaka kipindi cha miaka miwili na zaidi.
Aidha tathmini hiyo ya kupungua kwa magonjwa hayo iliambatana na kamati kutoa vitamin A kwa watoto wapatao 33,704 wenye umri wa miaka 5. Hata hivyo watoto waliopata chanjo ni 32,483 sawa na 103%, licha ya kufanya hivyo kamati ya lishe inategemea kutoa matone ya Vitamini A na dawa za minyoo kwa watoto chini ya miaka 5 kuanzia June 1 hadi June 30, 2019.
Mikakati mbalimbali iliwekwa na kamati hiyo ya kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wanajamii na kuvitembelea vituo vyenye changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya watoto wenye utapiamlo lakini pia kuwajengea uwezo watoa huduma ngazi ya jamii juu ya unasihi wa lishe .
Arusha- Namanga Road, Longido Town
Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha
Telephone: 027-2539603
Mobile: 0756395889
Email: ded@longidodc.go.tz
Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM