• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA WILAYA MHE. NURDIN BABU AMEKUTANA NA KAMATI YA MSINGI YA AFYA YA JAMII KUTOA ELIMU YA UVIKO-19 NA UMUHIMU WA CHANJO YA UVIKO-19

Posted on: September 27th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha Mhe. Nurudin Babu amekutana na kufanya majadiliano na viongozi wa Mila( Alaigwanani) pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali (dini) juu ya kuhakikisha wananchi wilayani hapa wanapata chanjo ya UVIKO 19.

Alisema Kumekuwa na baadhi ya wawakilishi wa wananchi kupotosha jamii dhidi ya chanjo inayoendelea kutolewa ya Johnson and Johnson (JANSSEN) na kupelekea wananchi kuingiwa na hofu na kukata kuchanja.

" Hakuna serikali duniani ipo kwa ajili ya kuua wananchi wake,na hata hapa kwetu Tanzania hakuna Kiongozi Yupo tayari kuua wananchi wake hivyo achaneni na Maneno ya wapotoshaji" alisema

Aidha alitoa angalizo kwa baadhi ya viongozi wenye tabia hiyo kuacha Mara moja kwani atawachukulia hatua Kali za kisheria ,huku akitoa agizo kwa wakuu wa idara ya elimu na afya kuhakikisha watumishi wote wa idara  hizo wanapata chanjo ili kuwalinda watu na wanafunzi wanaowahudumia au kuwafundisha.

Naye Kaimu Mkurugenzi Ndugu Edward Mboya alimuhakikishia Mkuu wa wilaya kuwa atahakikisha maagizo yote aliyotoa yanatekelezwa kwa wakati kabda ya zoezi hili kuisha kwa kuwahimiza watumishi wote wanaotoa huduma kwa jamii wanafuata taratibu zote za kujikinga na ugonjwa wa Korona UVIKO-19 na kuhakikisha wanapata chanjo ya UVIKO-19 hasa walimu na wahudumu wa afya.

Baadi ya wazee wa Mila walitoa maoni yao na kuzungumzia sababu ya jamii kukataa au kuogopa kuchanja ni Maneno dhidi ya chanjo hiyo kuwa inapunguza nguvu za kiume lakini pia tatizo kubwa ni jamii kukosa elimu dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO 19.

Hata hivyo viongozi hao wa Mila waliazimia kwa pamoja kuwa sauti ya jamii katika kukubali na kupokea chanjo hiyo,huku wakikiri kuwa ugonjwa huo upo na umeua watu wengi Sana hata ndani ya jamii na kumuahidi Mkuu wa wilaya kuwa watasaidia kueneza elimu juu ya umuhimu wa kupata chanjo kwenye jamii wanazotoka.

Kwa upande wao viongozi wa dini walisema watatoa elimu katika nyumba za ibada na kukemea vitendo vya baadhi ya viongozi wa dini wanaopotosha wananchi juu ya chanjo na kusema masuala yanayohusiana na afya waachiwe wataalamu wa afya wao wabaki na mambo ya kiimani.


Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt  Seleman Mtenjela alisema chanjo hiyo ni salama na wamefanikiwa kuchanja watu 867 sawa na asilimia  33 ya dozi iliyotolewa wilayani hapo,hata hivyo Kati ya hao waliopata chanjo hakuna aliyewahi kutoa taarifa Kama amepata madhara au kuwepo kwa taarifa za vifo.

" Maudhi madogo madogo yapo lakini ni ya kawaida kutokana na kitu kipya kinavyoingia mwilini, ikiwemo maumivu kiasi katika sehemu uliyochomwa sindano,uchovu,homa au baridi na maumivu ya kichwa" alisema.

Baadhi ya wananchi waliochoma chanjo hiyo wamekanusha uvumi kuhusu kupotea kwa nguvu za kiume na kusema wapo imara ,huku wengine wakisema hawajapata madhara yoyote ya kiafya.

Mwisho.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.