• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KAMATI YA SIASA YA MKOA YATUA LONGIDO

Posted on: March 23rd, 2023


Mwenyekiti wa CCM Mkoa ndugu Steven Zelote pamoja na kamati ya Siasa mkoa wa Arusha  wamefanya ziara wilayani Longido tarehe 22/03/2023 ambapo wametembelea miradi mbali  mbali ya maendeleo iliyopo Wilayani humo

Miradi iliyotembelewa ni kama ujenzi wa madarasa katika shule ya Engong'osunyai katika kijiji cha Ngereyani kata ya Tingatinga, ikiwa ni ujenzi wa madarasa pamoja na matundu ya vyoo, pia kamati ya siasa mkoa wa Arusha imetembelea ujenzi wa bweni la wavulana katika shule ya Sekondari ya Tingatinga ambalo limegharimu fedha takribani milioni arobaini za kitanzania bweni hilo linauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 120 kwa mkupuo mmoja, na liko katika hatua za mwisho za kukamilika ili kuanza kutumika, bweni hilo la wavulana linataraji kukamilika na kukabidhiwa  mnamo mwishoni mwa mwezi wa tatu vile vile kamati imekagua ujenzi wa Maktaba ambao mradi ulisainiwa tarehe 14 Juni 2022 mradi huo wa ujenzi wa maktaba umegharimu kiasi cha shilingi milion 62 kati ya hizo fedha kiasi cha shilingi milioni 52 zimetolewa na wafadhili wa mradi PROBONO na kiasi cha shilingi milioni 10 imetolewa na Halmashauri na kufanya ujenzi huo kutumia kiasi cha shilingi milioni 62 ili kumalika, ikiwa bado lina upungufu wa shelf za kuhifadhia vitabu na meza kwa ajili ya wananfunzi.

Naye mkuu wa shule Mr Palanjo ameiomba kamati ya siasa pamoja na serikali kwa ujumla kutengeneza uzio katika shule hiyo ili kuzuia uvamizi wa wanyama hususani tembo kwakuwa wamekuwa tishio kwenye shule hiyo, sambamba na hilo mkuu wa shule ameiomba serikali kumaliza tatizo la maji shuleni hapo kwani ndio changamoto kubwa inayosumbua shuleni hapo ukizingatia shule hiyo ni ya bweni na ina wanafunzi wengi, maji yaliyopo hayatoshi na hayo machache wanachi wa vijiji vingine wamekuwa wakipasua mabomba kwa ajili ya mifugo kabla hayajafika shuleni hapo

Pia kamati imetembelea ujenzi wa hospital ya wilaya ya Longido ambayo iko katika hatua za mwisho za kukamilika na tayari hospitali hiyo imepokea vifaa tiba mbali mbali kama vile mashine ya mionzi yaani X ray, utra saund pamoja na vipimo vingine aidha mwenyekiti wa kamati ya siasa ameuomba uongozi wa wilaya ya Longido kuongeza kasi katika ujenzi huo ili wananchi wapate huduma bora na kwa haraka

Pia kamati imepita katika shule ya sekondari ya Longido na kukagua ujenzi wa madarasa pamoja na ofisi ya walimu vile vile ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Longido ambalo nalo liko katika hatua za mwisho kukamilika.

Kamati ya siasa imehitimisha ziara yake katika mradi wa maji Namanga ambao umekuwa ukiwasambazia maji wananchi wa namanga na vitongoji vyake pamoja na uchache wa maji katika mradi huo wataalamu wa maji Auwasa wameimbia kamati kuwa wamepanga utaratibu wa kuchimba kisima kirefu kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo na kwa kuwa ni mradi mkubwa usaidia sana kuondoa changamoto ya maji ndani na nje ya Namanga.

Naye mkuu wa wilaya ya Longido mheshimiwa Marko Ng'umbi ameishukuru sana kamati ya siasa ya mkoa kwa kufanya Ziara katika miradi ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kusimamia vema na kwa uadilifu mkubwa ili iweze kumalika kwa wakati na kutumika kuwasaidia wananchi wa wilaya ya Longido na vitongoji vyake sambamba na hilo pia amemshukuru Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi mbali mbali kwenye halmashauri ikiwemo madarasa, mabweni, vyoo, pamoja na hospital na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo ya mkoa.

Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Mheshimiwa John Mongela amepongeza uongozi wa Halmasahauri ya walaya ya Longido kwa kazi nzuri kwani miradi yote iliyo tembelewa ni mizuri inaendelea vizuri, imesimamiwa vema na imeendana na thamani ya pesa iliyotumika ama kutolewa na serikali ya awamu ya Sita

Aidha mwenyekiti wa kamati ya siasa mkoa ndugu Steven  Amewaomba wanachama wa ccm  pamoja na wataalamu kufuata kanuni na taratibu za na pia kufuata muongozo wa katiba ya chama cha mapinduzi ikiwa moja ya ilani za chama ni kusimamia ukamilishwaji wa miradi inayotolewa na serikali kwenda kwa wananchi

Vile vile mwenyekiti wa CCM mkoa amewaasa wana Longido kuwa makini na utumiaji sahihi wa mitandao kwani matumizi yasio sahihi uleta uchochezi kwa jamii "Ndugu zangu wana Longido tujitahidi kumaliza changamoto zenu wenyewe bila kushirikisha mtu wa pembeni na iwapo itatulazimu kufanya ivyo basi tufuate utaratibu kanuni na sheria kwa sababu sheria zipo na ziko wazi" Alisema ndugu Steven Zelote

Aidha Mwenyekiti  huyo wa chama amemshukuru mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbali mbali yenye tija kwa wananchi "Kusimamia miradi vizuri na kukamilisha kwa muda uliopangwa itamsaidia Rais wetu kutuongezea fedha kwa miradi mingine mizuri yenya tija kwa wananchi kama barabara shule masoko pamoja na miundo mbinu mingine" alisema Stiven Zelote. Aidha amemaliza kwa kuwataka wanachama kufanya kazi kwa kushirikiana bila kuoneana ikiwa na lengo la  kumuunga mkono mama Samia na kusongesha gurudumu la maendeleo na kutimiza ilani za chama cha Mapinduzi.


*Jamhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee*

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM