• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KAMATI YA SIASA YAFANYA ZIARA YA MIRADI MBALIMBALI LONGIDO

Posted on: October 6th, 2021

Leo tarehe 06-10-2021 kamati ya Siasa wilayani Longido imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi iliyoko katika kata ya Sinya na Tingatinga ikiwemo Bwawa la Mifugo,kituo cha mawasiliano, ujenzi wa jingo la utawala na maabara ya Komputa katika shule sekondari Tingatinga na mradi wa Mizinga ya nyuki katika kata ya Tingatinga.

Katika ziara hiyo Katibu  wa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Enduiment (EWMA) wilayani Longido Mkoa wa Arusha Igno Laitayok amesema walipokea fedha shilingi billion 1.9 kutoka kwa Mfuko wa wanyamapori duniani (WWF) kwa ajili  kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF)katika jumuiya hiyo.

Akielezea miradi iliyotekelezwa kwa kamati ya Siasa ya wilaya (CCM) alisema miradi hiyo ililenga kubabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi pamoja na kudhibiti migongano baina ya wanyamapori na binadamu,ikiwemo ujenzi wa bwawa Endemwa lenye gharama ya shilingi million 106.

Alisema ujenzi wa bwawa katika mpaka wa kata ya Sinya na Olmolog utasaidia kupatikana kwa maji kwa mifugo na wanyamapori,na mradi huo umewekewa uzio ili mifugo wasiweze kuingia na kuharibu miundombinu lakini Kuna birika(cattletraff) kwa ajili ya kunyweshea mifugo na wanyama katika eneo la bwawa.

" Uwepo wa bwawa hili utapunguza migogoro baina ya wanyamapori na binadamu nyakati za utafutaji wa maji" alisema Laitayok.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Joseph Ole Sadira alipongeza na kuwashukuru wadau hao ,huku akitoa wito kwa halmashauri kuwapa ushirikiano wadau hao wakati wa utekelezaji wa miradi kwa manufaa ya jamii,hususani wataalamu wa Halmashauri hiyo.

" Miradi ya wafadhili ni mizuri kweli ,na hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha zao na ufuatiliaji,huko Kwa wafadhili hakuna wizi Wala ubadhirifu" alisema Ole Sadira.

Mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) Zakaria Faustin alisema wametekeleza miradi maeneo mbalimbali ikiwemo WMA ya Ikona huko Meatu ,lakini eneo lililopata miradi ya upendeleo ni EWMA,na halmashauri iliwapa ushirikiano wa kutosha.

" Hapa tumewapa miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa ofisi ya jumuiya shilingi millioni 427,000,000,Ujenzi wa kituo Cha utoaji wa taarifa za utali shillingi millioni 225,000,000 na kujenga kituo Cha Hali ya hewa shilingi millioni 20,000,000 hiyo ni mifano ya miradi" alisema Faustin.

Mkurugenzi mtendaji Ndg Stephen Ulaya naye aliwashukuru  Wadau hao kwani wameisaidia serikali kutekeleza mahitaji ya jamii “kwani kimsingi sisi serikali tulitakiwa kutekeleza haya hivyo basi fedha kidogo iliyotakiwa kuletwa kutekeleza mradi huu utaelekezwa sehemu nyingine kutatua changamoto za jamii yetu”.

Aidha , Mwenyekiti wa Halmashauri Simon Oitesoi alisema wafadhili hao wametekeleza majukumu ya halmashauri hiyo,na kuwaomba wasiishie hapo waendelee kusaidia serikali katika kutekeleza mahitaji ya wananchi.

Naye Mkuu wa Wilaya Nurudin Babu alisema wilaya hiyo ni ya kifugaji na uhifadhi hivyo miradi hiyo imelenga uhalisia wa eneo husika,na kueleza kuwa uwepo wa bwawa litasaidia kuondoa mwingiliano baina ya wanyamapori na binadamu katika makazi.

" Wanyama wakipata maji hapa hawataweza kwenda kwenye jamii kuleta taharuki kwani huduma zao zimesogezwa karibu na mazingira Yao"

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM