• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

KATIBU TAWALA LONGIDO ALIA NA WATENDAJI WA KATA .

Posted on: November 28th, 2023

Mheshimiwa Rahma Kondo Katibu tawala Longido amewataka watendaji wa kata kutoka kata zote kumi na nane za Wilaya ya Longido kuwekea uzito na umakini wa hali ya juu kwenye utendaji kazi wao hasa kuhusu swala zima linalotokana na lishe, Mheshimwa Rahma ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe ya robo ya kwanza cha tarehe 28/11 /2023 katika ukumbi wa J. K Nyerere Wilayani Longido.

Kikao hicho cha tathmini ya Mkataba wa Lishe kimehudhuliwa na wajumbe mbali mbali wakiwemo watendaji wa kata katika kata zote kumi na nane. Mheshimiwa Rahma amewaagiza watendaji kufanya maadhimisho ya siku ya Lishe kwenye kata zao ili kuifanya jamii kuondokana kabisa na tatizo la ukosefu wa lishe kwa wa mama wajawazito na watoto hasa wa chini ya miaka mitano na mara tu wanapofanya maadhimisho hayo kutoa taarifa kwa kamati tendaji zinazoshughulika na uwasilishaji wa taarifa hizo kwenye ngazi  husika yaani Mkoani na hatimae kwenye ngazi ya makao makuu OR Tamisemi. 

"Ndugu zangu hebu tulichukulie jambo hili kwa umakini mana tulisaini Mkataba hapa mbele ya Mkuu wa Wilaya, si hivyo tu Mkuu wetu wa Wilaya alisaini Mkataba na Mkuu wa Mkoa na kwa utaratibu huo nae Mkuu wa Mkoa aliingia Mkataba kwa ngazi za juu ya uongozi na jambo hili na la Mheshimiwa Rais mwenyewe Mama Samia Suluhu Hassan ambae ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe Taifa"Alisema Bi Rahma Kondo.


Akisoma taarifa ya Tathmini Mkataba wa Lishe Wilaya Ndugu Adelina Kahija taarifa imeonyesha kuwa Halmashauri ya wilaya ya Longido ina jumla ya watoto elfu ishirini na saba na mia nane na kumi na tatu, walio chini ya miaka mitano. Katika  kipindi cha Julai hadi Septemba 2023 jumla ya watoto 13497walifanyiwa tathmini ya hali ya Lishe kwenye vituo vya kutolea huduma ya Afya.

Tathmini ya hali ya Lishe katika Wilaya ilionyesha Kuwa 85.98% ya watoto chini ya miaka mitano wana hali nzuri ya Lishe na 13. 40% wana utapiamlo wa wastani na 0.61%wana utapiamlo mkali.Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imetenga kiasi cha Shilingi 51,084,500 kwa ajili ya utekelezaji wa Afua za lishe. Fedha zilizotengwa kutoka kwenye mfumo wa mapato ya ndani ni shilingi 37,490,000 na mfuko wa Afya ya pamoja shilingi 12,239,000,user fee 630,000 NHIF 500,000, na ICHF shilingi 225,000.

Kwa robo ya Kwanza Julai hadi Septemba 2023 Halmashauri ilipanga kutumia kiasi cha shilingi Milioni 10,904,000 ikiwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa Afua za lishe katika wilaya.

Akizungumza kwa niaba ya watendaji wa kata ndugu Kulunjuu N Laizer ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Daktari Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona na kutambua umuhimu wa lishe kwenye jamii hasa hii ya wafugaji waliopo kwenye Wilaya ya Longido na kuahidi kutekeleza yale yote yalio shauriwa na kujadiliwa kwenye kikao hicho cha Tathmini ya Mkataba wa lishe sambamba na kufanya maadhimisho ya Afua za lishe kwa kila kata husika ili wananchi wajue na kuwa na uelewa juu ya hali ya Lishe.

Nae Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Longido Ndugu Dominic Ruhamvya ameishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele swala hili la lishe kwa jamii, "Ndugu zangu hili jambo la lishe na la muhimu sana na kama tunavyotambua kwa umuhimu wake huo Mwenyekiti wa lishe Taifa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenyewe kwa maana hiyo basi tuweke mkazo sana kwenye kutekeleza shughuli hizi za lishe sambamba na kutoa elimu kwa jamii zetu ili wafahamu umuhimu huo wa lishe bora.

Vikao hivi vya Tathmini ya Mkataba wa  lishe ni endelevu ambavyo vinafanyika katika kila robo kwa mwaka.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KAZI IENDELEE.

Imetolewa na Happiness E Nselu 

Kaimu Afisa Habari Wilaya. 

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM