• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ZIARA YA KAMATI YA FEDHA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO..

Posted on: September 1st, 2023

Kamati ya fedha Utawala na Mipango imefanya ziara  ya siku 2  kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Afya, Elimu na  Barabara  inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Longido kwa siku mbili mfululizo  tarehe31/08/na 01/09 /2023. 

Utekelezaji wa miradi hii ya maendeleo katika Wilaya ya Longido inatekelezwa kwa Fedha zinazotolewa Serikali kuu, Kapu la Mama, BOOST, LANES II, TASAF, CDCF, SEQUIP pamoja na Mapato yake ya ndani zaidi ya Bilion 2.6 kwa ujumla wa fedha zote, ikiwa ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa Serikali katika kuleta Maendeleo kwa wananchi wake.

Kamati hiyo ya Fedha ya halmashauri ya Longido pamoja na wataalam wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Simon Oltosoi imetembelea na kujionea miradi takribani 24 yenye gharama ya zaidi ya Bilioni 2,602,688,130.53 inayotekelezwa Wilayani Longido.

Miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni Kituo cha Afya Gelai Lumbwa ambapo kamati imetembelea Ujenzi wa jengo la Mochwari, jengo la Upasuaji, Jengo la mama na mtoto, jengo la Wagonjwa wa nje pamoja na ujenzi wa jengo la maabara,

Miradi hii ya maendeleo kwa kiasi kikubwa ipo kwenye hatua za mwisho za ukamailifu wake ili iweze kutumika na kuwanufaisha wananchi waishio kwenye kata hiyo hata wa nje ya Halmashauri ya Longido, pia kamati imejionea  na kujiridhisha ujenzi wa kituo cha Afya Ketumbeine sambamba na nyumba ya watumishi 3 kwa  1 inayojengwa kwenye kata ya Ketumbeine,Miradi mingine iliyotembelewa ni kama mradi wa ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Mundarara, ujenzi wa madarasa Matatu shule ya Sekondari Tingatinga ,Jengo la Maktaba na Bweni katika sekondari ya Tingatinga, ujenzi wa shule Mpya ya sekondari Kamwanga,Ujenzi wa Shule ya Msingi Irkaswa, Ujenzi wa shule ya awali ya mfano Irkaswa, ujenzi wa nyumba ya watumishi Irkaswa ,  Ujenzi wa Matundu ya vyoo shule ya Msingi Lerang'wa sambamba na ujenzi wa madarasa matatu katika shule hiyo ya Lerang'wa pia kamati  imetembelea na kuona ukamilishwaji wa majengo shule ya Sekondari Sinya, Kamati imejonea ujenz wa barabara ya jamii yenye urefu wa km za mraba 3.6,ujenzi wa Stand ya Malori Eworendeke na  ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi iliyopo Longido.

Pia kamati imetembelea miradi inayofanywa na vikundi mbali mbali vya kinamama vijana na watu wenye ulemavu  vinavyonufaika na mikopo ya Halmashairi ikiwemo kikundi cha Juhudi kilichopo katika kijiji cha Longido na kikundi cha vijana Naibala Itubula katika kijiji cha Matale A, kikundi cha vijana Enyorata katika kujiji cha Irakaswa pamoja na kikundi cha wanawake kilichopo kijiji cha Gelai Lumbwa 

Vile vile kamati ya Fedha Utawala na mipango imetoa ushauri mbali mbali kwa wenyeviti wa kamati za utekelezaji wa Miradi na viongozi wa kisiasa katika kila Miradi inayotekelezwa wilayani hapo kuwa waone namna njema ya kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora na kufuata miongozo iliyowekwa na Serikali ,Pia jamii ihamasishwe kuchangia miradi ya Maendeleo.

"Waheshimiwa madiwani pamoja na wataalam sote kwa pamoja tunapaswa tuweke jitihada kubwa sana katika kuisaidia serikali juu ya Miradi tuliyopewa tunayo dhamana kubwa sana ya kuhakikisha tunaisimamia kwa weredi mkubwa sana mana miradi ni yetu sote sisi Wananchi wa Longido na Serikali kwa kutujali na kutupenda sisi wananchi wa Longido imetupatia  pesa nyingi sana kwenye kutekeleza Miradi hii basi tumsaidie mama Samia kwenye kusimamia utendaji wa kazi hizi kwemye Halmasahauri yetu kila mmoja wetu aone analo jukumu katika kusimamia utekelezwaji wa Miradi hii kwa manufaa wananchi wa Longido ili wapate huduma bora kwenye nyanja zote za Elimu Afya Maji na Hata barabara. "Alisema Mheshimiwa Simon Oitesoi.

Miradi yote ya Maendeleo iliyotembelewa na kamati hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za ukamilishwaji wake.


*Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kazi iendelee


Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM