• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

LONGIDO SASA TAYARI KUPATA MAJI SAFI MUDA WOTE

Posted on: July 8th, 2019

WIZARA Ya maji na umwagiliaji inatarajia kutoa shilingi million mia moja na saba(100.7 million ) kwa ajili ya ujenzi Wa miundombinu ya Mifugo kunywa maji( cattle turf)wilayani Longido Mkoa Wa Arusha,kwa lengo la kuondoa migogoro baina ya wafugaji na serikali juu ya uharibifu Wa miundombinu ya mradi Wa maji kutoka mto simba Wilaya ya siha Mkoa Wa Kilimanjaro uliogharimu zaidi ya sh16 billion fedha kutoka serikali kuu.

Akielezea katika  ghafla ya makabidhiano ya mradi huo  kutoka katika mamlaka ya  maji Wilaya ya Longido na kusimamiwa na mamlaka ya maji safi na usafi Wa mazingira  Mkoa Wa Arusha (AUWSA) Prof Kitila Mkumbo ambaye ni katibu mkuu wizara hiyo alidai kuwa ni uamuzi Wa serikali ikiwa ni sehemu ya agizo la Rais  Magufuli kuwa mamlaka zote za maji zijitegemee.

" Serikali imeamua kutenga sekta Hii ya maji kujitegemea ili ziweze kufanya kazi kwa kasi na kuhakikisha serikali za mitaa zinapata maji ikiwa na usimamizi mzuri ,akitolea mfano kama Tanesco ilivyo na  wakala wa umeme vijijini Rea pamoja na Tan Road ilivyo na wakala  ambao ni Tarura" alifafanua

Prof Kitila alisema Lengo hasa ni kuanzishwa kwa wakala Wa maji safi na usafi Wa mazingira vijijini,ikiwa ni kupanga na kusimamia uwezeshwaji Wa maji vijijini na sasa serikali ipo katika hatua ya kusimika mamlaka hiyo rasmi,hivyo mamlaka ya maji Longido kuanzia sasa itakua chini ya usimamizi Wa  mamlaka ya maji Mkoa Wa Arusha (AUWSA)

Aidha alidai kuwa changamoto kubwa katika sekta ya maji ni baadhi ya miradi ya miaka ya nyuma kutokukamilika kwa wakati kutokana na baadhi ya wakandarasi kushindwa kutekeleza majukumu yao ,akitolea mfano mradi wa maji mkoa wa kilimanjaro  ulioanza tangu mwaka 2014 lakini hadi sasa hauja kamilika

"Nawapongeza viongozi wote Mkoa Wa Arusha na hata ngazi ya Wilaya ya Longido,mradi Huu mmeusimamia vizuri ,lakini naomba hadi itakapo fika mwisho Wa mwezi Huu wale wote waliokua wamejiandikisha katika mpango Wa kupata maji waunganishiwe na kwa sasa wauziwe ndoo ya maji sh 20 wakati Mamlaka AUWSA ikiendelea na  mikakati  ya kupanga  bei kwa kushirikiana na Ewura" aliomba Prof Kitila

Hivyo Prof Kitila  ametangaza rasmi Leo mradi mkubwa Wa maji  kutoka chanzo cha maji mto simba wilaya ya siha mkoani kilimanjaro uliotekelezwa na serikali kuu   katika wilaya  ya Longido wenye thamani zaidi ya Shillingi  Billion 16 ikiwa ni fedha za ndani  umekamilika na utakua chini ya usimamaizi Wa mamlaka ya maji safi na usafi Wa mazingira Mkoa Wa Arusha (AUWSA)

Hata hivyo mkuu Wa Mkoa Wa Arusha Mrisho Gambo aliagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani  kwa watu 21 waliohusika kuhujumu mradi huo kwa kutoboa bomba za maji,kwani serikali imetoa fedha nyingi sana haiwezekani kuwavumilia wachache wanao haribu mradi huo

" Naagiza Mkuu Wa Wilaya kamata wale wote walio husika kutoboa mabomba na wafikishe mahakamani,Lakini pia niwaombe wananchi Wa Longido tunzeni mradi huu " Mhe. Gambo

Awali Mkuu Wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe alisema changamoto iliyopo kupitia mradi huo ni wananchi (wafugaji) kutoboa mabomba ili Mifugo yao ipate maji,na hali hii inasababishwa na ukame uliopo wilayani hapa,hivyo alisisitiza serikali kukamilisha ujenzi Wa mbauti ( cattle turf) ili Mifugo ipate maji kwa wakati.

Mkurugenzi Wa maji safi na usafi Wa mazingira Mkoa Wa Arusha (AUWSA) Mhandisi Ruthi Koya alisema Wilaya ya Longido ilikua na upungufu Wa maji safi na salama,lakini kupitia mradi huu maji safi na salama yapo na  yanatarajiwa kuhudumia watu elfu 26,142 ifikapo mwaka 2024

" Mji wa longido unawakazi elfu 16,712 kwa sasa hivyo bado kuna maji mengi ya ziada ,na lengo hasa la serikali nikuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama " Mhandisi Koya

Makabidhiano hayo yamehudhuliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido Mhe. Sambore Molloimet, Mkurugenzi mtendaji wa Wailaya hiyo Ndug. Jumaa Mhina pamoja na wakuu wa Idara zote zinazohusika na Mifugo na Uvuvi, Maji afi na Maji taka n.k.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM