• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

LONGIDO YAJA NA MPANGO MKAKATI DHIDI YA WANYAMA PORI

Posted on: November 19th, 2024

Na Happiness Nselu


Shirika la Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania (TPW) limeanzisha mpango mkakati wa kutoa mafunzo kwa jamii katika vijiji vya Kimokouwa na Eworendeke wilayani Longido, kwa lengo la kuimarisha usalama wa binadamu na wanyama pori.  


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Meneja wa Shirika hilo, Bw. Envis Kisimiri, alieleza kuwa changamoto za mwingiliano kati ya binadamu na wanyama pori zimeendelea kuongezeka, hasa ikizingatiwa kuwa Longido ni mojawapo ya maeneo muhimu ya makazi na mapitio ya wanyama pori.  


“Mafunzo haya yanalenga kuwasaidia wakazi wa maeneo haya kujua njia bora za kujikinga dhidi ya wanyama pori, huku tukihakikisha wanyama wanabaki salama. Tunataka kufanikisha ushirikiano wa kudumu kati ya binadamu na mazingira,” alisema Bw. Kisimiri.  


Shirika la TPW limeeleza kuwa mpango huu ni sehemu ya jitihada za muda mrefu za kupunguza migogoro inayotokana na mwingiliano wa binadamu na wanyama pori, ambayo mara nyingi huleta madhara kwa pande zote. Mafunzo haya yanatarajiwa kuwahamasisha wanajamii kutumia mbinu salama kama vile ujenzi wa vizuizi imara, ufugaji wa mbwa wa kufukuza wanyama hatari, na matumizi ya teknolojia njia ya kitamaduni na  kufuatilia mienendo ya wanyama pori.  


Kwa niaba ya wakazi wa Kimokouwa na Eworendeke, Bw. Elianis Salaashe amepongeza juhudi za TPW, akibainisha kuwa elimu hiyo ni ya msingi kwa usalama wa maisha na mali zao. Alisisitiza kuwa mwingiliano na wanyama kama simba na tembo umekuwa changamoto kubwa, na kwamba mafunzo haya yamewapa maarifa ya kukabiliana na changamoto hizo kwa njia endelevu.  


Bw. Salaashe aliongeza kuwa mafunzo haya pia yameimarisha uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi wanyama pori, si tu kwa usalama wao bali pia kwa faida ya kiikolojia na kiuchumi, ikiwemo utalii ambao ni chanzo muhimu cha mapato.  


Mpango huu wa TPW unatazamiwa kupanuka hadi vijiji vingine wilayani Longido, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, ili kufanikisha lengo la kuimarisha usalama wa binadamu na hifadhi endelevu ya wanyama pori. Pia, mipango ya ziada inajumuisha kuanzisha vikundi vya walinzi wa jamii kwa ajili ya kuimarisha usalama zaidi na kuendelea kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanajamii.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM