• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

Posted on: July 11th, 2025

Na Happiness Nselu 

Halmashauri ya Wilaya ya Longido imepokea tuzo ya pongezi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI baada ya kufanikisha lengo la ufaulu lililowekwa kwenye Key Performance Indicator (KPI) katika Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili kwa mwaka 2024.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa kwa mara ya kwanza wakati wa mkutano wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika Manispaa ya Iringa, ambapo Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI – Elimu, Ndg. Atupele W. Mwambene, aliipongeza Halmashauri ya Longido kwa mafanikio hayo ya kitaaluma.

Akizungumza katika kikao hicho, Ndg. Mwambene alisema kuwa Longido imeonyesha mfano wa kuigwa katika kusimamia taaluma, kuwajengea walimu mazingira bora ya kufundisha na kushirikisha jamii katika maendeleo ya elimu.

“Tumeona matokeo ya juhudi zenu. Longido ni miongoni mwa halmashauri zilizofikia viwango vya ufaulu tulivyovitarajia. Hili ni jambo la kujivunia,” alisema.

Mara baada ya kuwasili Longido, tuzo hiyo imekabidhiwa rasmi leo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw. Nassoro Shemzigwa, ambaye alipokea kwa niaba ya timu nzima ya elimu ya halmashauri hiyo.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Bw. Shemzigwa ameishukuru TAMISEMI kwa kutambua juhudi za halmashauri yake, na kusema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya mshikamano, nidhamu ya kazi na usimamizi mzuri wa walimu pamoja na viongozi wa elimu katika ngazi zote.

“Tuzo hii ni motisha kubwa kwetu. Itaendelea kutusukuma kufanya vizuri zaidi, si tu kwa Kidato cha Pili, bali katika nyanja zote za elimu,” alisema Shemzigwa.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka TAMISEMI, Longido imepanda kwa kasi katika viwango vya ufaulu ikilinganishwa na miaka ya nyuma, jambo linaloashiria ufanisi wa mikakati ya kuinua kiwango cha elimu vijijini.

Hii ni mara ya kwanza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido kutunukiwa tuzo ya aina hiyo, hatua inayoweka historia mpya na kuongeza hamasa kwa wadau wa elimu wilayani humo.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.