• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI WAIBUA MIKAKATI MIPYA YA KUBORESHA MAISHA YA WANANCHI WA LONGIDO

Posted on: November 11th, 2019

Leo tarehe 11-11-2019 wajumbe wa Baraza la madiwani wa halmashauri ya Longido wamefanya mkutano wa kawaida katika ukumbi wa JK Nyerere ulioko Halmashauri ya wilaya ya Longido. Mkutano huo ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bwana Gerson Mtera  na Mh Simon Oitesoi Diwani kata ya Gelai Lubwa ulikuwa na ajenda mbalimbali ikiwemo kupitia maazimio yote ya mkutano uliopita na utoaji wa taarifa wa utekelezaji wa kata kwa kipindi cha Julai mpaka septemba 2019.

Madiwani hao waliweza kuwasilisha taarifa hizo wakiwa wameeleza mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika nyanja za elimu, kilimo, ufugaji, utekelezaji wa miradi ya maendeleo , utunzaji wa mazingira ,kiuchumi na afya.

Katika uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji waheshimiwa wajumbe madiwani wa kata walitoa taarifa mbalimbali kutoka katika kata zao ikiwemo utekelezaji wa miradi mipya na inayoendelea, mafanikio , changamoto na njia za jinsi ya kutatua changamoto hizo.

baadhi ya changamoto zilizo bainishwa ni pamoja na utoro wa wanafunzi mashuleni, upungufu wa vyumba vya madarasa ,nyumba za watumishi yaani waalimu,  uhaba wa malisho ya mifugo, usafiri , maji safi na salama katika maeneo yao,madawati na vitendea kazi kwenye ofisi za umma.

Pia baraza la madiwani walimtaka afisa kilimo wilaya Ndugu Edward Kasiga kutoa vibali vya kupewa mahindi katika kata uzingatie uhitaji na sio kiwango kimoja kwa kata zote kwani kuna baadi ya kata hazina uhitaji na mwisho walikubaliana kuwa ugawaji wa mahindi ili kukabiliana na mfumuko wa bei katika kata mbalimbali ufanyike kwa kutegemea uhitaji wa kata husika  kwani kuna baadhi ya kata hazina uhitaji kabisa ya mahindi hayo.

Mkuu wa  wilaya ya Longido Ndugu Frank James  Mwaisumbe alipata nafasi ya kuongea kwa kifupi na alisisitiza baadhi ya mambo muhimu kama ujenzi wa vyumba vya madarasa, uanzishaji wa shule ya kidato cha tano na sita katika shule ya Endument kwa ajili ya kuhamisisha wanafunzi kupata nafasi ya kuchukua masomo ya sayansi. Pia mkuu wa wilaya alisisitiza ugawaji wa mahindi kwa bei nafuu ili kuepukana mfumuko wa bei kwa kuzingati uhitaji.

Mh Simon Oitesoi alifunga kikao saa 7.00 mchana kwa kupata chakula cha pamoja  na wajumbe wote.  

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM