• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu sekondari
      • Miundombinu, Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mjjini
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Utawala na Usimamizi wa Rasimamli Watu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • TEHAMA
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Utalii
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Leseni
    • Huduma za Utalii
    • Huduma za Mapato
    • Huduma zetu Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati ya Maadili ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Barua pepe za Idara na Vitengo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Kituo cha habari
      • Maktaba ya Picha
      • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
  • Vivutio
    • Mbuga
    • Ziwa

OPARESHENI YA JENGA CHOO TUMIA CHOO

Posted on: August 22nd, 2019

OPARESHENI YA JENGA CHOO TUMIA CHOO.

Mkuu wa Wilaya ya Longido , Mhe. Frank James Mwaisumbe ametoa agizo kwa maafisa Tarafa na watendaji wa vijiji vyote wilayani Longido kuwa anatoa miezi mitatu(3) tu,wahakikishe kila kaya (boma) ina choo, pamoja na sehemu zenye mikusanyiko ya watu kama vile sokoni, shuleni (msingi na sekondari).

Mh. mwaisumbe ameyasema hayo leo hii tarehe 22.08.2019 akiwa katika kikao cha afya na lishe kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mh mwaisumbe ameongeza kuwa  mtu yeyote atakaye kiuka agizo hili, kwa maana kuwa asijenge choo na kutumia choo atachukuliwa hatua za kisheria. 

Pia Mh. Mkuu wa wilaya amewaagiza maafisa elimu (msingi na sekondari) kuwasimamia   walimu wakuu wa shule na kuwahimiza mazingira kuwa safi na kuhakikisha kuwa wanatumia vyoo vizuri ili kuepuka uchafuzi wa mazingira na kuondokana na magojwa ya kuhara kama vile kipindupindu ndani ya wilaya yetu ya Longido. Amesema kuwa kufikia mwakani Longido haitakiwi kuwa katika namba ya 166 ndani ya wilaya 184 Tanzania kwani kila kitu kinawezekana tukiamua, Mh. Mwaisumbe amewataka maafisa tarafa kutoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa vyoo na matumizi yake kila baada ya mwezi mmoja. Pia amewaasa maafisa tarafa kushirikiana na idara ya afya pamoja na maendeleo ya jamii kuwa na ratiba ya kuelimisha jamii juu ya afya na umuhimu wa vyoo katika jamii.

Nae afisa afya mkoa wa Arusha Vones z Uiso ameeleza jinsi gani operesheni hii ya vyoo ilivyo weza kubadilika toka kuanzishwa mwaka 2012 hadi 2015. Amesema kuwa operesheni hii ya awamu ya pili mwaka 2017 hadi 2019 imekuwa na maendeleo mazuri mkoani Arusha hadi kufikia 81% kwa kuwa na vyoo.  Katika kuelezea changamoto ya afya  amesema kuwa mila na desturi potofu zimechangia jamii kutokuwa na vyoo, pia ameeleza uhaba wa maafisa wa afya katika ngazi ya mkoa kwani wana uhitaji wa watu 155 huku maafisa afya jumla wako 102 hivyo kuna changamoto katika kutaka kuwafikia watu wote katika kila kijiji na ndio maana wanaomba kusaidiana na watu wote ili kuwa na afya bora.

Pia Afisa lishe wilaya Adelin kahija ameeleza baadhi ya changamoto katika ngazi ya wilaya kama ukosefu  wa vitendea kazi kwa wataalamu wa lishe, ukosefu wa rasilimali fedha. Amesema kuwa anaunga mkono agizo la Mkuu wa wilaya kuhakikisha kila kaya ina kuwa na choo.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO September 04, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • VIONGOZI WA DINI WILAYA YA LONGIDO WATOA TAMKO JUU YA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

    October 23, 2025
  • WANAFUNZI 5,188 KUFANYA UPIMAJI WA KITAIFA DARASA LA NNE LONGIDO

    October 21, 2025
  • WWF YADHAMIRIA KUREJESHA MAZINGIRA ASILIA YA LONGIDO

    October 20, 2025
  • MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA PILI YA MAFUNZO YA WWF KWA VIONGOZI WA DINI, VIJIJI NA VIONGOZI WA KIMILA KUHUSU UHIFADHI WA MAZINGIRA LONGIDO

    October 16, 2025
  • View All

Video

KAMATI YA AMANI NA HAKI WILAYANI LONGIDO YATOA TAMKO LA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.