• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

RAS ARUSHA DKT KIHAMIA AWAFUNDA WATUMISHI WA WILAYA YA LONGIDO.

Posted on: October 7th, 2021

Katibu tawala Mkoa wa Arusha Dkt Athumani Kiamia leo tarehe 07-10-2021 amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Longido na kuongea na  watumishi katika ukumbi wa Halmashauri na  kuwataka watumishi wa Halmashauri ya Longido kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na taratibu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kupunguza malalamiko yanayojitokeza  katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali na kupunguza uonevu kwa watumishi

Alisema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo kwa lengo la kukumbushana wajibu wa utendaji kazi na kupokea malalamiko au changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Dkt Kiamia akizungumza Hali ya ukusanyaji wa mapato alisema wilaya hiyo bado Kuna Wigo mdogo wa ukusanyaji wa mapato na usiposimamiwa vizuri miradi ya maendeleo itashindwa kutekelezwa ipasavyo na kwa wakati.

Akifafanua juu ya fedha za makusanyo ya mapato ya ndani alisema fedha hizo ni za serikali kuu hazina tofauti na fedha za Ruzuku,na kuitaka halmashauri kutenga asilimia 40 ya mapato ya ndani kila mwezi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.

" Kwenye hiyo asilimia 40 ndani yake Kuna asilimia 10 ya makundi maalum ambayo ni Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu,Na fedha hizi zisipotolewa kwa makundi hayo tutahitaji maelezo" alisema Dkt Kiamia.

Katika hatua nyingine alisema utaratibu wa kubadili matumizi ya fedha Kama ilivyoelekezwa ni lazima kuandika barua kuomba kubadili matumizi bila ridhaa ni kosa na ulinganishwa na ubadhirifu wa fedha za Umma,hivyo aliwataka idara ya Mipango kusimamia vyema miradi ya maendeleo katika ngazi zote.

Hata hivyo alitoa agizo kwa wakusanyaji wa ushuru wanaodaiwa na halmashauri hiyo kuhakikisha wanarejesha fedha hizo haraka siku ya leo na kuwachukulia hatua wakusanya mapato wote wanaodaiwa fedha hizo.

" Nitawachukulia hatua,hapa Nimeona wanaodaiwa ni watu 27 nilishatoa maelekezo awali naona hayajatekelezwa , viongozi wakuu wa serikali akiwemo Waziri Mkuu anakemea ubadhirifu huu wa fedha za Umma ambao pia ni agizo la Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu" alisema Dkt Kiamia.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Stephen Ulaya alisema kuna baadhi ya wakusanya ushuru wadaiwa na wanaendelea kuzifuatilia kwa ukaribu sana ili ziweze kurejeshwa.

Naye  Mwanasheria wa Halmashauri Erick Justine alisema " Mh RAS tumechukua hatua na tunaendelea kuhakikisha fedha zinarejeshwa pia tumepokea ushauri wako wa kufanya kazi kwa taratibu na kuafuata miongozo ya serikali" alisema Justine

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.