• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Serikali yawahakikishia wafanyakazi ubora wa mafao.

Posted on: May 1st, 2018

Serikali wilayani Longido imewahakikishia wafanyakazi kuwa serikali sikivu ya awamu ya tano itahakikisha uunganishwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii unalenga kuboresha  mafao ya wafanyakazi na si vingenevyo.


Ahadi hiyo ya serikali imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya  ya longido Daniel G.Chongolo alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) iliyofanyika kiwilaya mjini Longido.


Chongolo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amesema serikali chini ya uongozi imara wa Rais John Pombe Magufuli  ilifanya uamuzi wa kutunga sheria ya uunganishaji wa mifuko hiyo ya hifadhi za jamii kwa lengo la kuongeza tija ya mafao kwa watumishi na kuepusha urasimu usiokuwa na tija.


Aidha akijibu hoja zilizotolewa na wafanyakazi kupitia risala yao, Mkuu huyo wa wilaya ya Longido amesisitiza kuwa serikali inatambua changamoto nyingi zinazowakumba wafanyakazi wake, zikiwemo za kupandishwa vyeo, madai ya malimbikizo ya madeni, uhaba wa nyumba za watumishi pamoja na changamoto za mazingira magumu ya kazi na kuwahakikishia kuwa serikali inazifanyia kazi changamoto zote ili kuwafanya watumishi wabakize wajibu wa kutenda kazi pekee.


Changamoto ambazo zimeanza kutatuliwa ni pamoja na kulipwa kwa madeni ya watumishi zoezi lililoanza mwezi Machi 2018, ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika maeneo ya pembezoni, pamoja na uboreshaji wa mazingira ya kazi kwa ujumla.


Kwa upande wake Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Longido Mikidadi Ally amewakumbusha waajiri  wa serikali na sekta binafsi kuwa kisheria chini ya kifungu cha 31 cha matumizi mabaya ya madaraka ni kosa la jinai kutokupeleka michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii.


Maandimisho ya Mei Mosi mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo "Uunganishwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii ulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi".

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM