• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SHEREHE YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE KIMKOA YAFANYIKA WILAYANI LONGIDO

Posted on: October 1st, 2019

Leo tarehe 01-10-2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya Longido imefanyika sherehe ya kuhitimisha kilele cha siku ya wazee ambayo kimkoa imefanyika hapa wilayani Longido na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Ndugu Toba Nguvila ambaye ni katibu tawala wa wilaya pamoja na wazee wote kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Arusha. Kwenye maadhimisho hayo wazee walipata nafasi ya kusoma risala fupi mbele ya mgeni rasmi ndugu Toba nguvila ambayo ilielezea hali ya wazee kimkoa na kiwilaya, mambo ambayo wanatekeleza kama baraza, mikakati na changamoto mbalimbali wanazozikabili kama ifuatavyo;-

Mheshimiwa Mgeni rasmi.

Awali ya yote nipende kumshukuru Mungu kwa kukuwezesha kuungana nasi kwenye tukio hili muhimu kwa wazee wetu, Hakika umeacha majukumu mengine na kulipa jukumu hili kipaumbele.

Huduma za ustawi wa jamii zimekuwa zikiratibu pamoja na mambo mengine masuala ya wazee , kwa kuzingatia sera ya Taifa ya wazee ya  mwaka 2003, Sera ya Afya 2007 na Miongozo mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha wazee wanastawi vyema na kupatiwa fursa sawa pasipo kubaguliwa kwa namna yeyote ile.

Maadhimisho ya mwaka 2019 Kitaifa yanafanyika Mkoani Mtwara na yamebeba kauli mbiu isemayo “TUIMARISHE USAWA KUELEKEA MAISHA YA UZEENI”. Ujumbe huu una maana kubwa sana hasa ukizingatia kumekuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili unaopelekea wazee wetu kukosa uangalizi na kuwa kundi lililotengwa, kama kutakuwa na usawa na malezi bora kwa wazee hatutegemei kuwa na makao ya wazee kwani wazee ni vizuri wakalelewa katika ngazi ya familia, kwani uzee na kuzeeka hakuna wa kuukwepa.

  • Uzee ni hatua ya Mwisho ya ukuaji kutoka utotoni, kulingana na Sera ya Taifa ya Wazee ya 2003 na Sera ya Afya (2007).Hivyo basi, Mzee ni mtu yeyote mwenye umri wa miaka 60 na kuendelea. Pia Sheria ya Utumishi wa umma pia inatambua kuwa miaka 60 ni umri wa kustaafu na ukistaafu kwa mujibu wa sheria wewe ni Mzee. Na katika kanuni za kudumu za utumishi wa umma za mwaka 2009 kifungu Namba 43 (1) nacho kinasisitiza  juu ya umri huo katika kustaafu.

     MAMBO YALIYOTEKELEZWA

Tumeendelea Kuhamasisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa Wazee kwa kuweka matangazo katika  hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati yanatoa ujumbe  usemo ‘MZEE KWANZA: MPISHE MZEE APATE HUDUMA’ ikiwa ni njia ya kutoa huduma kwa haraka kwa Mzee katika vituo vyetu vyote vya huduma.

Jumla ya mabaraza 548 kati ya 687 yameundwa katika ngazi mbali mbali ndani ya Mkoa wa Arusha kuanzia ngazi ya Kijiji/Mtaa hadi ngazi za Mkoa sawa na asilimia 80%.

Mkoa umeitikia agizo la kuwatambua wazee kama ilivyo kwa makundi mengine muhimu nchini mwetu na Hadi sasa jumla ya wazee 64,999 wametambuliwa ,

Mkoa umefikia 52% ya utoaji wa vitambulisho kwa wazee na tumeazimia ifikapo mwezi March 2020 kila Halmashauri iwe imekamilisha zoezi hili kwani fedha zimetengwa kwenye mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Jumla ya wazee 8 na maafisa ustawi 4 wameweza kushiriki katika maadhimisho ya wazee Kitaifa Huko Mkoani Mtwara ambapo Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mgeni rasmi.

Mkoa umeweza kuwapatia wazee Ofisi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za Baraza.

BARAZA LA WAZEE MKOA

Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 inasisitiza kwamba “YATAUNDWA MABARAZA YA USHAURI WA WAZEE KATIKA NGAZI ZA VIJIJI/MITAA, KATA, WILAYA, MKOA NA TAIFA”

Mnamo tarehe 08/12/2018 Mkoa uliendesha kikao maalum cha uchaguzi wa baraza la wazee ambapo jumla ya Halmashauri tano (5) kati ya saba (7) zilishiriki na kuchagua uongozi wake

Baraza la wazee mkoa wa Arusha linaundwa na jumla ya wazee 49 yaani wazee saba kutoka kila Halmashauri, na linaviongozi saba wakiwemo mwenyekiti, makam, katibu, makamu, mhazini, na wazee wawili Me na Ke.

MAJUKUMU YA BARAZA

Mwongozo na majukumu ya mabaraza ya wazee ngazi ya vijiji/mtaa, kata, wilaya, mkoa na taifa unafafanua juu ya hili kupitia matamko na vifungu mbalimbali kwenye sera ya wazee kama inavyoonekana

Ibara ya 3.14-.3.15 na, Sura ya 4, Ibara ya 4.1 – 4.4)

Kufanya Mkutano wa Baraza la Wazee la Mkoa kila baada ya miezi 6. Kwa maana hiyo Baraza la Mkoa litakutana Mara mbili (2) kwa Mwaka.

Kusimamia utoaji wa huduma kwa Wazee katika halmashauri zote.

Kuhimiza Halmashauri, Asasi na Wakala za Hiari ili kutoa huduma mbalimbali za msingi kwa Wazee wote wa miaka 60 na kuendelea.

Kushauri Serikali kuwa na mwakilishi wa Wazee kwenye Bunge kama ilivyo kwa makundi ya wanawake, Walemavu na vijana.

Kupokea kero mbalimbali za Wazee kutoka kwenye halmashauri zote na kuzitafutia ufumbuzi.

Kuchagua wawakilishi wawili watakaoshiriki katika kuunda Baraza Huru la Wazee la Taifa.

Kuratibu shughuli za Mabaraza ya Wazee ya kila halmashauri na lile la Mkoa

Kushiriki na kutoa mawazo kwenye vikao, mikutano na hafla mbalimbali ngazi ya mkoa.

Mabaraza yatadumu kwa muda wa miaka 3

CHANGAMOTO

Pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mkoa na Serikali ya Tanzani kwa ujumla kwa kushirikiana na wadau katika kutoa huduma stahiki  kwa Wazee, bado eneo hili linakabiliwa  na  changamoto ambazo zinahitaji kushughulikiwa kwa pamoja:

Uchache wa Maafisa Ustawi wa Jamii kwenye ngazi ya Halmashauri hasa kwenye kata na vijiji ambako hakuna Afisa Ustawi wa jamii hata mmoja, Wilaya ya Longido ina afisa ustawi wa jamii mmoja tu ambapo leo tunaadhimisha siku hii muhimu.

Baadhi ya Halmashauri Kutokutenga vyumba na madaktari mahsusi wa kutoa huduma za Afya kwa wazee kwenye Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati

Upatikanaji duni wa madawa kwa ajili ya magonjwa ya Wazee  na huduma za Mkoba kwa Wazee

Uchache wa wadau katika eneo la Wazee na Walemavu.

Ufinyu wa bajeti za masuala ya wazee na huduma za Ustawi wa Jamii ngazi za Halmashauri

Kutokamilika vitambulisho vya wazee kwa baadhi ya halmashauri kama jedwali lilivyoonyesha hapo juu kwani ni 52% tu ndio wenye vitambulisho.

3:  MIKAKATI 

Kuhakikisha mabaraza ya wazee Mkoa na Wilaya yanapatiwa mafunzo juu ya majukumu yao, kwa sasa tupo kwenye mazungumzo na wenzetu wa Helpage kuona namna ya kuratibu na kuwezesha mafunzo haya.

Uongozi wa wazee kushawishi masuala ya wazee kujadiliwa katika vikao muhimu kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya ili kuongeza msukumo wa utekelezaji wa mahitaji yao.

Kuhakikisha zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya Wazee unakamilika katika Wilaya Zote hasa (Karatu na Longido) ambapo takwimu zinaonyesha wapo chini.

Kuwahimiza wazee kuunda vikundi vidogo vidogo vya kijasiriamali na kifugaji kwa ajili ya kuzalisha mali jambo ambalo litawasaidia kupata mahitaji yao madogo madogo ya kila siku.

HITIMISHO

Tunakushukuru wewe binafsi kwa kukubali kuungana nasi katika siku hii muhimu kwa wazee wetu, Nitoe shukrani pia kwa Viongozi wote wa Mkoa, wilaya na Halmashauri kwa ushirikiano waliouonyesha kufanikisha sikua hii, kipekee niwashurkuru viongozi wa baraza la wazee Mkoa ambao jitihada zao za kuona siku hii inafanyika hapa Wilayani Longido zimezaa matunda.

Mwisho Ndugu mgeni rasmi alimalizia kwa maneno machache akisema

Ninapenda kuwatakia kila la kheri katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwezi November na ninaamini tutashiriki vyema na kutumia haki yetu ya Kikatiba vizuri, ninaahidi kushirikiana na Viongozi wote wa Baraza kwa Lengo la kuboresha huduma kwa wazee wetu ndani ya Mkoa wetu,

Nawashukuru wazee kwa kunipa jukumu la kulea baraza la wazee Mkoa baada ya kuniomba wakati wa uzinduzi ninawaahidi kazi, pia Ninawashukuru wote walioandaa maadhimisho haya, wakiwemo Viongozi wa wazee, Mganga Mkuu wa Mkoa na Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya kwa kuwawezesha baadhi ya wajumbe mliopo hapa kufika, pia wataalam wa serikali hasa maafisa ustawi wa jamii kwa kushiriki kwenu kikamilifu mwenyezi mungu awabarika sana.

Tunazitambua juhudi hizi kama mchango katika kuwajali wazee na ninaomba ziendelezwe pia niwaombe kwa namna ya kipekee tuendelee kuliombea Taifa letu na viongozi wetu chini ya Mh Rais Dr John Pombe Magufuli ili kazi nzuri anayoifanya iendelee kuboreka na wananchi wetu waendelee kustawi vyema tunapoelekea kwenye uchumi wa kati.


 

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM