• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI ZIMEWANUFAISHA WACHIMBA MADINI MUNDARARA

Posted on: December 2nd, 2019

Wilaya ya Longido katika kuadhimisha kilele cha  siku ya Ukimwi Dunia inayofanyika Tarehe 01-12-2019 kila mwaka leo Tarehe 02-12-2019 imefanya sherehe ya  kuadhimisha  kilele cha siku ya Ukimwi Duniani  katika eneo la wazi lililopo katika kata ya Mundarara.sherehe hizo iliyohudhuriwa na mgeni rasmi Ndugu Toba Nguvila akimwakilisha mkuu wa wilaya Mhe Frank Mwaisumbe, pia walihudhuria watumishi wa idara ya afya na maendeleo ya jamii wilaya, mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia, viongozi wa vijiji na vitongoji na viongozi wa dini.

Pia kwenye sherehe hizo zilizohudhuriwa na wananchi wengi wa kata hiyo hasa wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya Rubi ziliambatana na utoaji wa elimu juu ya Ugonjwa wa UKIMWI,upimaji wa afya na burudani kutoka katika vikundi mbalimbali vya dini, vijana na akina mama kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Longido.

Katika sherehe za MAADHIMISHO hayo yaliambatana na upimaji wa afya walijitokeza takribani zaidi ya wananchi mia tatu 300 kupima afya zao kwa hiari.

Mgeni rasmi Ndugu Toba nguvila akiwa kwenye sherehe hizo aliwahasa Sana wananchi wa Mundarara juu ya umuhimu wa kuadhimisha sherehe hizo na kuwapongeza Sana wananchi na viongozi wao kwa kuhudhuria kwenye sherehe hizo. Moja ya faida hizo Ni kutoa elimu kuhusu ugonjwa hatari wa UKIMWI ikiwa pamoja ya jinsi gani mtu anaweza kupata maambukizi,jinsi ya kujikinga na maambukizi na Kama utakutwa na maambukizi Ni jinsi gani unaweza kuishi kwa matumaini.

Kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema kuwa hakuna maambukizi mapya Bali tunajikinga kuzuia ueneaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI ndugu mgeni rasmi aliwataka wananchi kuacha kuendelea Mila potofu ambazo zinachangia ueneaji wa ugonjwa huu ikiwemo ukeketaji na kuoa wake zaidi ya mmoja. Pia aliwataka wananchi kumrudia Mungu wao katika Imani zao Kama wameshindwa kabisa kujizuia kutumia njia hizi potofu.

Nae kiongozi wa Mila Laingwanan alipata Nafasi ya kuielimisha wananchi waliohudhulia katika sherehe hizo na kuwasisitiza wananchi wa jamii ya kimasai kuacha kabisa ukeketaji na ndoa za wake zaidi ya mmoja kwani ndio Mara nyingi zinasababisha ueneaji wa ugonjwa wa UKIMWI.

Afisa maendeleo wilaya Bi Grace mghase aliwata wananch KUJITOKEZA kwa hiari kwenda kupima afya zao kwani kufanya hivyo kutawafanya kuwa na uhakika kabisa wa afya zao na kuwaomba kuacha KUWANYA NYAPAA wale ambao wanakutwa na virusi vya UKIMWI kwani kufanya hivyo kutawafanya wawe huru kwenda kupima afya zao kwa kujua kwamba jamii haitaninyanyapaa hata Kama nitagundulika na virusi vya UKIMWI.

Mwisho dokta Matrona mwakilishi wa mganga mkuu wilaya dokta Justice Munisi nae aliwataka wananchi kuwa na tabia ya kwenda kwenye vituo au zahanati kupima afya na sio kusubiri mpaka kwenye siku ya maadhimisho. Pia aliwashukuru wananchi wote kwa kujitoa kwenye siku hiyo na kuonyesha muitikio mkubwa na kwenda kupima afya.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.