• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA (SHIVYAWATA) LAFANIKIWA KUKUSANYA MILIONI 5.

Posted on: September 2nd, 2019

Leo tarehe 02/09/2019 shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu nchini Tanzania wilaya ya Longido (SHIVYAWATA)  imeandaa hafla katika kata ya Mundarara iliyohudhuriwa na mgeni rasmi  Mkurugenzi mtendaji hamashauri ya  wilaya ya Longido Ndugu Jumaa Mhina,pamoja na viongozi mbalimbali akiwepo Diwani wa kata hiyo ndugu Alais Mushao,watendaji na wenyeviti wa vijiji, Pia hafla hiyo iliyoambatana na harambee ya uchangiaji fedha ilisimamiwa vizuri kabisa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Jumaa Mhina na kufanikisha kukusanya kiasi cha Tshs. Milioni tano (5,000,000/=) kwa ajili ya uboreshaji wa huduma mbalimbali zinazofanya na shirikisho hilo kuwasaidia watu wenye ulemavu wanaoishi katika  wilaya yetu  ya Longido.

Aidha Mkurugenzi mtendaji hamashauri ya  wilaya ya Longido Ndugu Jumaa Mhina alisimama na kusema pongezi kubwa kabisa ziende kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Raisi wetu Dr John Pombe Magufuli kwa kuamua kutenga asilimia kumi 10% ya vijana,wanawake asilimia mbili 2% iende kwa walemavu, pia amesema mwaka huu wameshatoa kiasi cha Tsh milioni mia na  thelasini mbili (132,000,000/=) tayari kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu. Pia mkurugenzi mtendaji aliwataka jamii ya watu wenye ulemavu  kutengeneza vikundi kwa ajili ya kuwasaidia kupata mikopo hiyo isiyo na riba asilimia 2% kwani fedha hizo zitawasaidia katika kujikwamua na ugumu wa Maisha.

Pia katika hafla hiyo mwenyekiti ndugu Elisha Maala Millya wa shirikisho  la watu wanaoishi na ulemavu wa aina mbalimbali ikiwemo viungo vya mwili, ulemavu wa Ngozi na kuona taklibani elfu tatu na mia tano (3,500) katika wilaya Longido alisoma risala fupi ikielezea changamoto na mafanikio mbalimbali ambayo wameyapata tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa shirikisho hilo ndugu Elisha Maala Millya alibainisha baadhi ya Changamoto wanazozipata watu wenye ulemavu zikiwemo:- kunyanyapaliwa, kutokuwa na ofisi maalumu, kutowapeleka Watoto wenye ulemavu shuleni, swala la ajira, changamoto ya usafiri, ubovu wa miundo mbinu sio Rafiki kwao na mwisho alimalizia na kutokuwepo na bajeti ya kutosha kwa watu wenye ulemavu wilaya ya longido.

Pia mwenyekiti ndugu Elisha Maala Millya alibainisha baadhi ya mafanikio ambayo wameyapata Tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo yakiwemo ;- kupatiwa mikopo ya asilimia mbili 2% na kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali, kupata baiskeli hamsini (50) aina ya wheelchairs kutoka katika kampuni ya Tanzania Big Safari, kupata ofisi eneo la orbomba japo inahitaji ukarabati kidogo pamoja na samani za ofisi, kufanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa wilaya yetu, kukutana na watu wenye ulemavu kutoka katika kata mbalimbali za wilaya ya Longido na kuweza kufanya vikao mara tatu kwa mwaka kama katiba ya a shirikisho inavyosema.

 Mwisho mwenyekiti ndugu Elisha Maala Millya alimalizia kwa kutoa shukrani nyingi kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kujali sana watu wenye ulemavu kwa kuteuliwa wizara ya watu wenye ulemavu pia kuwashirikisha katika ngazi mbalimbali zikiwemo uwaziri,ubunge pamoja na ubalozi,pia kututengea asilimia mbili 2% ya pato la serikali kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya watu wenye walemavu. Pia kumshukuru mkurugenzi mtendaji Ndugu Jumaa Mhina kwa kuweza kufika katika hafla hiyo kwa kuacha  majukumu mengine ya kiofisi na kuja kuhudhuria hafla hiyo na  kufanikisha kupatikana kwa kiasi cha fedha Tsh milioni tano (5,000,000/=). 

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.