• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Uhasibu
      • Mipango na Uratibu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu,Mipango ya Maendeleo ya Vijijini na Mijinii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Usafishaji na Mazingira
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Uchaguzi
      • Maliasili na Utalii
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Rasilimali Asili na Hifadhi ya Mazingira
      • Usimamizi wa Taka na Usafi wa Mazingira
      • Ufuatiliaji na Tathmini
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Maliasili na uhifadhi wa mazingira
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Leseni
    • Mapato
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,Afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti UKIMWI
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango Mkakakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Vikundi vya wanawake,vijana na walemavu vyaendendelea kunufaika na mikopo isiyokuwa na Riba

Posted on: October 16th, 2019

Leo tarehe 16/10/2019 Halmashauri ya wilaya ya Longido imeendeleza desturi yake ya kutoa Mikopo kwa makundi mbalimbali ya walemavu, wanawake na vijana ikiwa ni agizo la serikali ikitaka kila Halmashauri kutenga asilimia 10% ya mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi hivyo.

Jumla ya vikundi 17 vilivyomo ndani ya wilaya ya Longido vimenufaika na mkopo huo wa takribani milioni hamsini (50,000,000/=) uliotolewa na halmashauri.

Afisa maendeleo ya jamii wilaya Bi Grace Mghase alisema wilaya ya Longido ina takribani vikundi 541 vilivyosajiliwa ikiwemo 11 watu wenye ulemavu, 105 vijana na 425 wanawake vyote hivi vinajishughulisha na uzalishaji mali na vyote vinaratibiwa na kusimamiwa na idara ya maendeleo ya jamii. Pia alisema kuwa halmashauri inaendelea kutekeleza agizo la serikali la asilimia 10 ya mapato ya ndani kurudishw kwa jamii kwa kuwapatia mkopo usio na riba. Mwisho alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri ilitoa mkopo wa kiasi cha shilingi 132,630,000 kwa vikundi mbalimbali na mwaka huu wa fedha 2019/2020 wamepanga kutoa kiasi cha shilingi 150,000,000 ya pato la ndani.

vikundi vilivyonufaika na mkopo huo ni pamoja na Msanja – Namanga, Naserian Olokii - Ngereyani, Kipok Tengai B-Merugoi, Amani -Kamwanga, Namunyak -Mundarara, Juhudi -Longido, Kiserian -Oltepes, Nashipai - Lubwa, Tumaini -Kiserian, Ilanywaak – Ilerai, Nasyeku -Orkrjuloong, Dupoto – Owerendeke, Namanga Vijana Unity -Namanga, Memusi -Lumbwa, Kikundi cha Esupat Kitendeni -Kitendeni, Pamoja walemavu -Kitumbeine, na Kikundi cha walemavu Engusero -Engusero

Akikabidhi cheki ya kiasi cha shilingi milioni hamsini 50,000,000 taslimu mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Longido Mh. Frank James Mwaisumbe, amesema Vikundi 17 mliopatiwa mkopo huo tayari fedha zenu zimeingizwa kwenye akaunti na Nawasihi mkatumie kwa jinsi mlivyo ainisha kwenye shughuli zenu bila kuathiri malengo ya vikundi vyenu na kurudisha fedha hizo kwa wakati ili na vikundi vingine viendelee kunufaika. Pia aliwaagiza watendaji wa mikopo kuhakikisha vikundi ambavyo vimeshapatiwa mkopo wasijirudie mpaka vikundi vingine nao wapate kwanza.

Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido  Ndg.Nestrory Dagharo ,amesema Vikundi vimepata mkopo wa jumla ya shilingi millioni 50 kwa ajili ya vikundi mbalimbali vya halmashauri ya wilaya yetu ,Nawasihi mkatumie kwa jinsi mlivyo ainisha kwenye shughuli zenu bila kuathiri malengo ya vikundi vyenu .

"Vile vile halmashauri itaendelea kutoa mikopo kwa vikundi vingine mbalimbali katika halmashuri yetu hivyo basi nawasihi mkafanye kazi na mrudishe mkopo kwa wakati ili na vikundi vingine viendelee kunufaika"alisema kaimu mkurugenzi Nestory.

Nae Mbunge wa Longido  Mh Steven Kiruswa amewaasa wanavikundi kutumia fursa hii vizuri wa ajili ya kuleta maendeleo na kubadilisha hali yao ya maisha. Pia Mbunge alishauri kuwa Vile vikundi ambavyo vitarudisha mkopo wake kwa wakati wapewe vipaumbele kwenye awamu nyingine ya mkopo ili kuwahamasisha vikundi vingine kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

Pia vikundi hivyo kumi na saba 17 walipata nafasi ya kupewa semina ya ujasiriamali kutoka kwa mtaalam Mkurugenzi Isaak Mnyangi wa shirika la integrity Foundation Society. Wanavikundi wamefundisha vitu na mbinu mbalimbali za ujasiriamali kama vile kutengeneza batiki na kuwaasa wajasiriamali hao kuweza kujiajiri ili kuondokana na umasikini na utegemezi. Amehimiza kuwa vyanzo vya vya umasikini nchini ni kutokana na watu wengi kutokujishugulisha katika kazi mbalimbali pamoja na kutotumia fursa wanazo pata.

Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA June 13, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    August 07, 2025
  • WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WILAYANI LONGIDO WALA KIAPO CHA UADILIFU

    August 05, 2025
  • SHIRIKA LA MONDO TANZANIA LAKABIDHI MAGODORO 32 KWA WANANFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU SHULE YA MSINGI LONGIDO

    July 30, 2025
  • LONGIDO YANG'ARA KITAIFA YAPATA TUZO YA UFAULU KIDATO CHA PILI

    July 11, 2025
  • View All

Video

LONGIDO YASHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE MAONESHO YA NANE NANE YANAYOFANYIKA VIWANJA VYA THEMI - NJIRO ARUSHA
More Videos

Kurasa za Karibu

  • ESS-Watumishi Portal
  • Staff Email

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved.