• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maulizo |
    • Barua pepe |
Longido District Council
Longido District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Longido

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya jamii
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Afya
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Ushirika
      • Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
        • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Teknolojia ya habari, mawasiliano na uhusiano
      • Ukaguzi wa ndani
    • Kata
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu ,afya na Maji
      • Kamati ya kuthibiti Ukimwi
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili ya madiwani
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • miradi iliyokamilishwa
  • Machapisho
    • sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • mpango mkakakati
    • Riport mbalimbali
    • Form mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA RASMI KAZINI WAAPISHWA LEO

Posted on: December 2nd, 2024

Na Happiness  Nselu 

Longido, Arusha - Viongozi wapya wa serikali za mitaa katika Wilaya ya Longido wameapishwa rasmi leo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, watendaji wa halmashauri, na wananchi waliokuja kushuhudia tukio hilo muhimu.

Hakimu mfawidhi wa Wilaya ya Longido  Mh.Eliarusia R.Nassary aliwaongoza viongozi hao katika kiapo cha uadilifu na uwajibikaji. Akizungumza baada ya kuwaapisha,Bw. Joseph Logolie aliwahimiza viongozi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uwazi, na kushirikiana na wananchi katika kusukuma mbele maendeleo ya jamii zao.


“Uongozi ni dhamana, na jukumu lenu kubwa ni kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wananchi wenu. Msikilize matatizo yao, tafuteni suluhisho kwa kushirikiana, na hakikisheni mnazingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma,” alisisitiza Bw Logolie.


Viongozi walioapishwa ni pamoja na wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji, na wajumbe wa halmashauri kundi la wanawake pamoja na wajumbe kundi mchanganyiko mbalimbali  Pia walikabidhiwa nyaraka muhimu zinazowaongoza kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na mwongozo wa usimamizi wa miradi ya maendeleo na utawala bora.


Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Mwenyekiti mpya wa Kijiji cha Orkojoolengush Bw.Lekshon Kaika Mollel  aliahidi kuwajibika kwa moyo wa dhati na kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kuboresha maisha ya jamii.


Kufuatia kuapishwa kwao, viongozi hawa wanatarajiwa kuanza mara moja kusimamia shughuli za maendeleo katika maeneo yao, kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya kuhakikisha Longido inaendelea kupiga hatua katika nyanja za kijamii na kiuchumi.


“Kwa pamoja tutaweza, na Longido itaendelea kuwa mfano wa kuigwa katika uongozi na maendeleo,” alihitimisha Bw. Joseph



Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA ASILIMIA 10% January 30, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 09, 2023
  • Uchaguzi wa kidato Cha tano 2023 June 11, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2023
  • View All

Habari Mpya

  • DED LONGIDO AFUNGUA MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

    May 14, 2025
  • MITUNGI 50 YATOLEWA KWA BABA NA MAMA LISHE WILAYANI LONGIDO

    April 17, 2025
  • WATAALAMU WA AFYA WATOA ELIMU KUHUSU MPOX KATIKA SHULE YA SEKONDARI ENGARENAIBOR NA KETUMBEINE

    March 21, 2025
  • WWF NA BBC MEDIA ACTION WATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA JAMII JUU YA UHIFADHI WA MAZINGIRA

    March 21, 2025
  • View All

Video

Ujenzi wa madarasa 4 na Ofisi ya walimu shule shikizi Lopoloseki,
More Videos

Kurasa za Karibu

  • Ufugaji
  • Elimu msingi Primary Education

Kurasa za zinazoshabihiana

  • Tovuti kuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Mkoa wa Arusha

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Arusha- Namanga Road, Longido Town

    Postal Address: S.L.P 84 Longido Arusha

    Telephone: 027-2539603

    Mobile: 0756395889

    Email: ded@longidodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maulizo
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 Longido DC . All rights reserved. Designed by Loth Zacharia & Joseph Peter Mkumbwa Sponsored by GWF TAMISEM